Stori: Mayasa Mariwata
MAHABAT! MKALI wa sinema na muziki wa Bongo Fleva, Baby Joseph Madaha amesema anatamani kuwa na mtoto lakini bado hajamuona mwanaume wa kuzaa naye na kuanika vigezo vya mwanaume anayestahili kuwa baba bora kwake.
Akibonga mawili matatu na paparazi wetu, Baby alisema suala hilo linahitaji umakini mkubwa katika uchaguzi na sifa anazozihitaji yeye ni upendo wa kweli na uhodari wa chumbani katika uwanja wa mahaba.
“Namsaka mwanaume mwenye sifa za kunizalisha, awe baba bora maana ishu ya kumpata mwanaume huyo si suala la mchezo lazima uwe makini ili mtoto wako ajivunie kwa mzazi aliyenaye, sichagui rangi ila awe mrefu na mwili uliojijenga, akiwa amenizidi umri au mdogo
freshi tu ilimradi aweze kazi,” alisema Baby.
Kwa umakini gani ulionao wewe Baby Madaha mbona wewe mwenyewe choko tuu...haya tafuta basi wanaume wapo kibao. Na kama ni suala la kuzalishwa maanake wewe una mimba tayari nenda hospitalini madaktari na manesi wakuzalishe lakini kama ni suala la kupewa mimba hata wapiga debe mbona wanaweza tuu coz nao ni wanaume saaana tuu
ReplyDelete