CHADEMA Yalaani Kufukuzwa Chuoni Waziri Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi Philipo Mwakibinga

Chama cha Demokrasia na Maendeleo-CHADEMA kimelaani vikali uongozi wa Chuo kikuu cha Dodoma kwa kumfukuza chuoni mtetezi mkuu wa wanafunzi ambaye ndiye waziri mkuu wa serikali ya wanafunzi Philipo Mwakibinga.

Taarifa kutoka ndani ya chama hicho kikuu cha upinzani nchini zinasema viongozi wakuu wa chama hicho wanalaani tabia ya kufukuza ovyo viongozi wa serikali za wanafunzi ili kuwaziba mdomo.

Philipo Mwakibinga ni mwanachama machachari wa Chadema na aliwahi kugombea Uenyekiti wa Bavicha Taifa.

Inaaminika Mwakibinga amefukuzwa kwa sababu ya Itikadi yake kisiasa.Na haya ni maelekezo ya uongozi wa CCM mkoa wa Dodoma kwa viongozi wa chuo hicho wakiamini kufanya hivi ni kuwatisha wanavyuo wasijiunge na Chadema.

Taarifa zaidi zinasema Kiongozi wa upinzani bungeni Freeman Mbowe amemeiagiza wizara ya Elimu kipitia Waziri Kivuli Suzane Lyimo kufuatilia kwa ukaribu suala hili ili kulinda haki za wanachuo hawa.


Updates.......

Maneno ya Philipo Mwakibinga aliyosema huku akiwa amezungukwa na polisi zaidi ya 500 ni haya :

""Nitarudi tena kusoma UDOM as soon as possible.Nitawashangaza Ulimwengu kwakuwa Mlacha na Kilua hawanielewi kama habari za Wagalatia.Lakini naamini makaburi yao na vizazi vyao vitakuja kunielewa hata kama miaka 20 ikipita.

Nawapenda wana UDOM Naipenda UDOM.TETEENI HAKI.KIVULI CHANGU KITAISHI TU.By Mwakibinga P.J.""""

Baada ya maneno hayo aliingizwa ndani ya gari ya polisi huku akisindikizwa na msururu wa magari zaidi ya 10 ya polisi na kuondolewa ndani ya eneo la chuo huku yeye akitabasamu na kuwapunguia mkono wanafunzi wenzake.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kamhamishieni SAUT, UDOM ni chuo cha umma

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad