Dada wa Diamond Queen Darleen Achochea Bifu la Diamond na AliKiba 'Machupa kiboko yake Pesaa'

Mwanamuziki ambae ni dada na Diamond Platnum Queen Darleen amezidi kuchochea chuki na bifu kwa mashabiki wa Ali Kiba na Diamond Platnum baada ya kupost maneno ambayo mashabiki hao wanaona ni kama anazidi kuchochea bifu iliyopo kwa mashabiki wa wanamuziki hao ambao kwa sasa wamekuwa na ushindani mkubwa kimuziki.

Mwishoni mwa wiki iliyopita kulikuwa na show kubwa ya muziki ambayo ilifanyika katika viwanja vya Ledears Club ambapo katika show hiyo iliwakutanisha Diamond Platnumz pamoja na Ali Kiba ambao kila mmoja alipata mapokezi tofauti kutoka kwa mashabiki wao.

Katika show hiyo kuna baadhi ya mashabiki ambao walikuwa na furaha kushuhudia show ya wakali hao wawili wakati show inaendelea msanii Diamond Platnum aliweza kuwarushia noti za buku mbilimbli mashabiki wake.Kufuatia kitendo hicho ndipo msanaii Queen Darleen amefunguka na kusema kuwa dawa ya machupa stejini ni pesa. "Machupa kiboko yake pesaa,tunasaka hela na wewe saka "

Mashabiki wa Queen Darleen wameonyeshwa kutofurahishwa na kauli ambayo imetolewa na dada wa nyota wa muziki Diamond Platnum na wao wanaamini kuwa msanii huyo anazidi kuchochea bifu iliyopo kwa mashabiki wa Diamond pamoja na Ali Kiba

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. acha ushabiki wa kijinga wewe

    ReplyDelete
  2. Na yeye roho inamuuma ndugu yake kurshiwa machupa, yeye aliyeandika na hao waliorusha machupa nani anachochea bifu? Kwa sababu Kuna siku uwanja wa burudani utageuka wa vita mashabiki wa D watachoka msanii Wao arushiwe makopo kila siku hili jambo linachukuliwa mzaa ipo siku yatatokea madhara makubwa

    ReplyDelete
  3. ACHA KUOMBA CORABO

    ReplyDelete
  4. Mdau hapo juu umenena....Anonymous 29,2015 at 2:32PM

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad