Sweetbert Lukonge na Ibrahimu Mussa
MOYO wa mshambuliaji Emmanuel Okwi ulisimama kwa sekunde kadhaa alipogongwa kisogoni na beki Aggrey Morris wa Azam FC.
Okwi aligongwa katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC iliyomalizika kwa sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, jana.Daktari wa Simba, Yassin Gembe, amesema moyo wa Okwi ulisimama kwa sekunde kadhaa kutokana na pigo la kisogoni karibu kabisa na ubongo katika eneo la Medullar Oblangata.
“Hakikuwa kitu kidogo, tulilazimika kufanya tiba ili kurudisha mapigo ya moyo wake kwa kuwa ulisimama kwa sekunde kadhaa. Aliumia na uliona akitoa mapovu. “Baada ya hapo, tuliona ni vema kumfikisha Muhimbili ambako vipimo vyote vimefanyika. Imeonekana hakuumia sana na ameruhusiwa.
“Lakini mimi nimeamua kumpumzisha kwa siku mbili ili kuangalia kama atakuwa katika hali gani maana mwanzo unaweza kuona yuko vizuri kumbe kuna tatizo. “Ikionekana anaendelea vizuri, basi ataanza mazoezi lakini atakuwa chini ya uangalizi wangu,” alisema Dk Gembe.
Mshambuliaji wa Simba, Dan Sserunkuma alitumia muda mwingi kumlaumu Morris kwamba alishiriki kumpiga Okwi kiwiko, hata hivyo, alikuwa akikanusha.Okwi alibebwa haraka na kutolewa uwanjani na baadaye kukimbizwa Muhimbili ikiwa ni baada ya kuzinduka.
Kugongwa huko kwa Okwi, jana jioni kulizua gumzo kwa mashabiki wa soka nchi hasa wa Simba ambao walikuwa wakipiga simu katika ofisi za gazeti hili wakidai mabeki wamekuwa wakatili kwa washambuliaji.
Wengi walitolea mfano wa beki George Michael wa Ruvu Shooting kumkaba mshambuliaji Amissi Tambwe wa Yanga.
wana simba tushirikiane kumuombea okwi
ReplyDeleteSio wanasimba tu jamani,
DeleteSema wote wenye roho safi tumuombee Okwi.