Msanii anayetesa katika mziki wa kizazi kipya hapa nchini, Nassib Abdul 'Diamond Platnumz' usiku wa jumamosi iliyopita alijikuta katika wakati mgumu baada ya kuzomewa na mashabiki kwenye viwanja vya Leaders Jijini Dar es Salaam.
Mbali ya kuzomewa, Diamond pia alirushiwa chupa za maji ambazo zilileta kadhia, lakini Diamond alionekana akiwahimiza madancer wake wafanye kazi iliyowapeleka pale licha ya zomeazomea kuzidi uwanjani.....
Msanii huyo alipoona vitendo vya kutaka kumkwamisha asiimbe vikiendelea, aliamua kuwamwagia fedha mashabiki hao, ndipo wakaacha kuzomea na kuanza kugombea fedha hizo kisha kuanza kumshangilia....
Baadhi ya wadau walisikika wakidai, kundi hilo lililokuwa likimzomea liko upande wa mmoja wa wasanii mahiri hapa nchini.Wasanii wengine walioonja joto ya jiwe ni pamoja na Khamis Mwinjuma 'Mwana FA' na Ambwene Yesaya 'AY'.
Aidha, baadhi ya mashabiki walilaani vikali tukio hilo la kumzomea Diamond na kumrushia chupa za maji ambazo inadaiwa zilikuwa na haja ndogo ndani yake.
Mashabiki hao walisema tukio hilo halipendezi na linapaswa kukemewa na kuwataka waratibu pamoja na jeshi la polisi kuzidisha ulinzi katika matamasha makubwa kama hayo.
Hii ni mara ya pili kwa Diamond kuzomewa,tukio la kwanza likiwa kilele cha tamasha la Fiesta mwaka jana kwenye viwanja hivyo.
Hao watu wa Udaku njoo wanamfanya Diamond azomewe.
ReplyDeleteOK, kwahiyo kila atakapo zomewa atakuwa akimwaga pesa. Kama Domo kagundua dawa ya wazomeaji na kumbe na wazomeaji nao wamegundua dawa ya kupata pesa - ngoma droooooooooo!!
ReplyDeleteHata wafanye nini bado nyota ya nguli hiyo imo juu,,kama maulana amepanga hakuna atakayepangua.....mwisho walila kwa diamond au makao....watu wasio na la kufanya ndio wanayoyafanya hayo....fools always remain fools....Diamond bado atapanda tu mpende msipende....ni wakati wake ngoje wake wenu ama waambulie tu kuzomea na kwenda kushi vichumba vya kupanga....
ReplyDeleteNyie ndio mnataka sasa azomewe kila show watu wakitaraji kurushiwa pesa
ReplyDeleteAcha tuzomèe tupate nauli
ReplyDeleteTatizo la watanzania ni ushamba umetuzidi, badala ya kuwapa support wasanii wetu wanaotuwakilisha vizuri nje ya nchi eti tunazomea kwa kumfurahisha mjinga mmoja aliyeshindwa music na kutafuta soko la kimataifa. Huyo kima wenu anatakiwa akubali matokeo kuwa muda wake ulishapita alishindwa kuitumia nafasi yake, sasa hivi akae pembeni ausome tena mchezo unaendaje na kuongeza bidii kwenye game siyo kutafuta watu wa kuzomea, hiyo haisaidii, kwani wazomeaji wote ni wale mamburula wasiojielewa. Ni hayo tu, mtake mistake Domo kawadizi na kuzomea siyo dawa, someni mchezo mwenzenu anafanyaje hadi kafika hapo, punguzeni wivu nyie bongo flevar na njama zenu za kishamba.
ReplyDeletehahahahaaa we bwege hapo juu unalalamika hadi unatia huruma
ReplyDeleteinaelekea domo anajupumuliaga vizuri kisogon
hahahahaaa we bwege hapo juu unalalamika hadi unatia huruma
ReplyDeleteinaelekea domo anajupumuliaga vizuri kisogon