Dida na Edzen, Baada ya Kuachana Sasa ni Marafiki Damu Damu, Minong'ono ya Kurudiana Yasambaa

Edzen na Dida 
Stori: Gladness Mallya
WATANGAZAJI ambao walikuwa wanandoa kabla ya kuachana, Khadija Shaibu ‘Dida’ na Ezden Jumanne wamemaliza tofauti zao na sasa wamekuwa marafiki sana kiasi cha kuzua minong’ono kwamba wamerudiana.

Baada ya minong’ono hiyo kuzidi, Risasi Vibes ilimtafuta Dida ili kueleza ukweli ambapo alisema ni kweli amemaliza bifu na Ezden na sasa ni marafiki lakini suala la kurudiana siyo kweli na halipo kabisa kwani tayari yeye ana mtu wake na Ezden pia ana mtu wake.

“Tumemaliza vinyongo tulivyokuwa navyo na sasa tuko kama watu wa kawaida lakini hakuna mapenzi tena na hatuwezi kurudiana. Pia kila mtu ana uhusiano mwingine, sisi ni marafiki tu watu waelewe hivyo,” alisema Dida.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. huyu demu mwenyewe kibibi, nadhani alidanganywa akatoka sasa hivi anaona ni bora angebaki ndani tu maana hakuna mwanaume anaweza kumchukua tena. tarehe ya kuharibika imeshapita huyu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad