Elimu ya Sekondari itakuwa BURE kuanzia 2016 - Jakaya Kikwete

Katika Salaam za Mwaka Mpya Kutoka kwa Rais Jakaya kikwete Amegusia Swala la elimu na Kusema kuhusu Elimu ya Secondary Mwaka ujao itakuwa ni Bure.

Nanukuu kama Ifuatavyo:

'Sera Mpya ya Elimu na Mafunzo
Ndugu wananchi;
Mafanikio mengine tuliyopata mwaka huu ni kukamilika kwa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014. Hii ni hatua muhimu sana katika maendeleo ya elimu nchini hakuna badala yake. Sera mpya inalenga kuinua ubora wa elimu na mafunzo na kuweka mifumo na taratibu zitakazowezesha Watanzania wengi zaidi kupata fursa za elimu iliyo bora na inayolinga na wakati tulionao. Jambo jipya sana na la kihistoria katika Sera mpya ya Elimu ni dhamira ya Serikali ya kuondoa ada katika elimu ya sekondari kuanzia mwaka 2016. Mpaka sasa hatuna ada kwenye shule za msingi, sasa wakati umefika kufanya hivyo pia kwa elimu ya sekondari. Kwa mujibu wa maelezo hayo ya Sera, nimekwishatoa maagizo kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Wizara ya Fedha na Tume ya Mipango kuanza kutafakari namna jambo hilo litakavyotekelezwa.' Jakaya Kikwete

~udakuspecially.com
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wezi wakubwa nyie mnauma na kupuliza wadanganyeni halo hao ambao hawajui tofauti,mmeiba mamilioni ya dollars alafu saa hizi mnawarubuni watu eti na elimu ya bure?????

    ReplyDelete
  2. Wezi tu hawa anasubiri miaka yote mlioiba hamkushtukiwa mpaka sasa mmeshtukiwa mnataka elimu iwe bure mlikuwa wapi miaka yote hiyo,mnaomba msamahaa ili watu wasahau.

    ReplyDelete
  3. Hakuna kitu kama hicho, labda hao wezi/mafisadi (CCM) waache kutawala hii nchi.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad