Habari Kamili ya Chanzo cha Panya Road Kufanya Vurugu Jana Jijini Dar Hichi Hapa

KIKUNDI kinachodaiwa kuwa Panya Road kimetikisa maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam kwa kupora mali, kujeruhi watu na kuzua sintofahamu katika maeneo ya jiji hilo wakiwa na mapanga mikononi.

Maeneo yaliyokumbwa na dhooruba hiyo ni pamoja na Sinza, Tandale, Mwananyamala na maeneo mengineyo usiku huu. Maduka na baa zimefungwa na kupelekea polisi kupiga risasi hewani kuwatawanya watu waliokuwa wamekaa kimakundimakundi.
Imeelezwa kuwa fujo zilianzia mchana leo baada ya kiongozi wa Panya Road aitwaye Diamond kuuawa maeneo ya mpakani mwa Tandale na Mwananyamala darajani usiku wa kuamkia mwaka mpya kwa kukatwakatwa na mapanga.

Baada ya kumzika mwenzao leo, vijana hao wakajipanga kwa ajili ya kufanya fujo.
Usiku ulipoingia wakaanza kazi na kusababisha taharuki kwa wakazi wa Jiji la Dar.
Baadhi ya mashuhuda walioshuhudia matukio hayo wanadai vijana hao walikuwa na silaha mbalimbali yakiwemo mapanga na walivamia maeneo kadhaa zikiwemo baa.
Wateja waliokuwa katika baa ya Calabash iliyopo maeneo ya Mpakani, Mwenge walilazimika kuacha vinywaji vyao na kukimbia hovyo huku wengine wakikanyagana na kukatwa na vipande vya chupa kwa kile kilichodaiwa kuwa vijana hao walikuwa wanakatiza maeneo hayo japo hawakuingia ndani.

Baada ya tukio hilo wateja wengi waliamua kurudi majumbani kutokana na baadhi yao kujeruhiwa na vipande vya chupa wakati wakikimbia.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad