Juma Nature na Inspekta Harun ni wasanii wa muziki wa kizazzi kipya waliofanikiwa kuwa na ushawishi mkubwa sana kwenye tasnia ya bongo fleva kipindi fulani kilichopita. Ni wasanii ambao kila mmoja kwa nafasi yake walifanikiwa kuandika rekodi mbalimbali zilizowafanya kuwa juu sana kimuziki.
Juma nature alifanikiwa kuweka rekodi ya maudhurio makubwa katika maonyesho ya uzinduzi wa album zake za ‘Nini Chanzo’ na ‘Ugali’. Pia alifanikiwa kwenye mauzo ya album zake na kuweza kufanya show nyingi sana ndani na nje ya Tanzania.
Inspekta Harun akiwa kama solo na memba wa kundi la ‘Gangwe Mob’ walifanikiwa kujaza watu wengi sana wakati wa uzinduzi wa album yao ya ‘Simulizi la Ufasaha’ na kuweka rekodi ya kipekee. Kupitia kundi lake waliweza kumiliki design za nguo zao zilizokwenda kwa jina la Gangwe Gear na website yao vitu ambavyo ni vikubwa sana kwa nyakati izo kufanywa na msanii wa kibongo na Afrika ya mashariki.
Inspekta Harun anakumbukwa kwa vibao vyake vilivyotamba kama ‘mtoto wa geti kali’, ‘Maisha ya uswazi’, ‘Asali wa moyo’, ‘Pamba nyepesi’ na vingine vingi alivyoimba mwenyewe au kwa kushirikishwa.
Juma Nature anakumbukwa kwa hits zake kama ‘Mgambo’, ‘Sitaki demu’ ‘Inaniuma sana’ ‘Hakuna kulala’, ‘Kighetogheto’ na nyinginezo.
Juma Nature na Inspekta Harun walikuwa ni wasanii wanaoshabiiana mambo mengi, kuanzia uhandishi wa nyimbo zao unaoelezea maisha halisi ya uswahilini na kiasi kikubwa namna ya kughani ambapo walitumia staili iliyojulikana zaidi kama ‘rap katuni’, pia maeneo wanayotokea ambayo ni ya uswahilini haswa, na ata pilika zao wakati wanaanza muziki inasemekana walishawahi kuangaika pamoja kwa namna moja au nyingine.
Kushabihiana uku kulipelekea washabiki wao kujaribu kuwalinganisha na kuwapima uwezo wao wa nani ni zaidi ya mwingine. Hii ilichochea kuibua mtafaruku baina ya wasanii wawili, wakatofautiana mpaka wakaunda makundi kwa washabiki wao ambao walikuwa wanajaribu kuwashindanisha . Mgogoro ukakuwa zaidi ukichochewa na vyombo vya habari pamoja na vijembe walivyorushiana kwenye nyimbo zao.
Baada ya ushindani na mgogogro uliofukuta baina yao kwa muda mrefu,wakaaamua kuweka chini tofauti zao na kufanya kazi ya pamoja chini ya mtayarishai nguli P Funk Majani.
‘Mzee wa busara’ ni kazi waliyofanya pamoja Inspekta Harun na Juma Nature, kazi iliyopokelewa vizuri sana na washabiki wa bongo fleva, na ikageuka kuwa gumzo kila kona ya Tanzania. Ni kazi iliyowaunganisha pamoja awa mahasimu wawili wakageuka kuwa marafiki,na pia ikawaunganisha pamoja na mashabiki wao kwa ujumla. Lengo ilikuwa kufanya albam ya pamoja kitu ambacho ata ivyo hakikufanikuwa. Nachoweza kusema ‘mzee wa busara’ ni moja ya nyimbo zilizosaidia kuisukuma tasnia ya muziki wa kizazi kipya kwenda mbele zaidi.
Leo hii ukizungumzia muziki wa bongo fleva,watu wanausimamisha ni mastaa wawili Ali Kiba na Diamond Platnumz. Diamond na Ali Kiba ni wasanii ambao kila mmoja amefanya mambo makubwa na kujizolea mashabiki wengi. Ni wasanii wanaofanya kazi nzuri na zinazopendwa ndani na nje ya Tanzania.
Ali Kiba ana hit songs kama ‘Cinderela’, ‘Nakshi nakshi’, ‘Hadithi’, ‘Far way’, ‘Single boy’ ‘mwana’ na nyinginezo. Kiba amefanikiwa kufanya maonyesho kwenye nchi mbalimbali za Ulaya na Marekani, amefanikiwa kufanya kazi moja na mwanamuziki nguli wa Marekani R Kelly.
Diamond Platnumz, amefanikiwa kutengeneza nyimbo zilizotamba sana kama ‘Kamwambie’, ‘Mbagala’, ‘Mawazo’,’Nitarejea’,’Kesho’ na ‘Number one’ ‘Mdogo mdogo’. Amefanikiwa kufanya maonyesho makubwa ndani na nje ya nchi pia amefanya kazi na wasanii wakubwa wa Afrika kama D Banj, Davido, Iyanya na wengineo.
Inspekta na Nature walifanya wimbo wa pamoja ukawa gumzo,ila hawakufanikiwa kutoa album. Itakuwaje kama Ali kiba na Diamond watafanya sio tu wimbo wa pamoja bali album nzima? Naamini itaweka rekodi ya aina yake ambayo haijawahi tokea kwenye muziki wa kizazi kipya. Kisha baada ya hapo tuwaone kwenye ziara ya pamoja sehemu mbalimbali. Tuwaone na mashabiki wao ambao ni wengi sana wakiunganika kuwaunga mkono kwenye kazi zao za pamoja. Na kuzidi kuusukuma mbele muziki wetu wa Tanzania kimataifa.
Muziki wa sasa ni biashara kubwa na kwenye biashara hakuna uadui wa kudumu. Penye fursa watu wanaojua biashara uweka tofauti zao kando na kutumia fursa kutengeneza faida. Nje ya kutengeneza faida Diamond na Kiba wana naafasi ya kutengeneza historia mpya na ya kipekee kwenye muziki wa nyumbani na kuzidi kuupa nguvu na ushawishi muziki wetu. Naamini hakuna kinachoshindikana.
By GadoTz/Jamii Forums
Itakuwaje kama Ali Kiba na Diamond wataamua kuwa Juma Nature na Inspekta Harun wa zama
2
January 10, 2015
Tags
Itakuwa ni njema sana A&D wakipatana na kufanya kazi pamoja coz vipaji vya viko juu sana,,,,,,,,,pleeeeeeeeez guys solve your tofauti mtafanya njema kinyama
ReplyDeleteBig point sana tu! Kama wanajitambua watafanyia kazi maoni yako
ReplyDelete