JB Aweka Wazi Jinsi Anavyompenda Mke Wake na Kuithamini Ndoa Yake

Mwigizaji na mwogozaji wa filamu za hapa bongo, Jacob Stephen ‘JB’ amefunguka ya moyoni  juu ya upendo wake kwa mke wake na kuendelea kudumisha ndoa yao.

JB tofauti na mastaa wengi wa hapa bongo, amemuweka na kumwambia waziwazi mke wake wa ndoa maneno  ya upendo ambayo huwafanya mashabiki wake wote kkujua na kumtambua shemeji yao au wifi yao.

JB leo hii ameweka picha hiyo mtandaoni akiwa na mke wake na kuandika maneno haya;

“Mke wangu,rafiki yangu, nampenda sanaa. Siku kama ya leo tuliingia kanisani tukatoa kiapo cha maisha,hakuna kilicho badilika wala kitakacho badilika mpaka kifo kitakapo tutenganisha. NAKUPENDA SANA MKEWANGU,Mungu azidi kuibariki ndoa yetu”. JB alimaliza.

Tunakupongeza JB kwakuendelea kuheshimu na kuitunza ndoa yako, tunawatakia baraka katika maisha yenu.
~Bongomovies
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. BIG UP KAKA MKUBWA!!!

    ReplyDelete
  2. ..... ujinga huo JB.. unamwanika mkeo ngoja wamuone wenye mate ya fisi:" wakubwa, waheshimiwa, wenyenazo" usije kutulilia hapa baadae. Wanene wa nchi hii wanataka kila kizuri kiwe chao...

    ReplyDelete
    Replies
    1. wewe acha wivu mpongeze ana mke mzuri basi

      Delete
    2. Acha ushamba ,kwani ukimficha akitaka kuliwa hataliwa?au hujasikia wako watu wanaliwa hata na wafanyakazi wao?
      JB mkeo mzuri sana.

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad