JB ambaye amefanya kazi kubwa katika kuiinua tasnia hiyo alisema, filamu inaangukia katika kifo kama ulivyoanguka muziki wa Bongo Fleva kutokana na soko kushikiliwa na maharamia.
Staa huyo alisema hali hiyo inawafanya wasambazaji kuanza kuikimbia tasnia hiyo na wengine kushusha bei ya filamu.
“Hali ya soko kwa sasa ni mbaya sana kwani uharamia umezidi, kwa mtazamo wangu najua tunaelekea mwisho, hata kitendo cha msambazaji mkubwa kama Steps kuamua kushusha bei ni kutapata na kujaribu kukuruka kutokana na hali ilivyozidi kuwa mbaya.
“Wasambazaji wa muziki walikuwa wakiwalalamikia maharamia kwa kuwazidi nguvu na serikali ikabaki kimya bila ya kuyafanyia kazi malalamiko yao, kama inavyofanyika katika filamu sasa,” aliongeza.
Katika mtazmo wake, JB anaamini kwamba suala la kushusha bei ya filamu wakati maisha yanapanda ni kifo cha tasnia hiyo inayopendwa na Watanzania wengi.
~BongoMovies