Mastaa wengi wamekuwa wakiutumia mtandao wa Instagram kupost picha ambazo zinaonesha maisha yao na karibia kila wanachofanya, lakini kwa msanii wa R&B Juma Jux kuna mstari ambao ameuweka kati ya vitu anavyoshare kwenye mtandao huo na maisha yake binafsi.
Inafahamika kuwa Jux anasoma nchini China, lakini hajawahi kupost picha yoyote ikionesha yuko kwenye mazingira ya chuo kama ambavyo labda hupost akiwa kwenye bata au akiwa na washkaji zake au kwenye show.
Baada ya kuulizwa kama kuna mambo mengine anayoyafanya huko tofauti na chuo, na kama kweli anasoma ni kwanini hajawahi kushare na mashabiki wake picha zozote za mazingira ya chuo, haya yalikuwa majibu yake.
“Nachoamini mimi hapa unajua mimi katika maisha yangu, Instagram ni profile yangu mimi naamua nifanye nini sifanyi kwasababu ya watu, pia najua mimi ni msanii kuna watu wananiangalia kuna vitu flani siwezi kuvuka nikavifanya, “ Jux aliiambia 255 ya XXL ya Clouds Fm.
“Darasani sio sehemu ya kupiga picha umuoneshe mtu, kwanza darasani kwetu hairuhusiwi kupiga picha, haiwezi kuwa mwalimu yupo anafundisha halafu unapiga nioneshe watu, no. Nazingira yangu ya nje ya chuo ndio nafanya vile haya ni maisha yangu ya nje ya chuo, lakini chuo nikienda naenda kusoma siendi kupiga picha, kama mtu haniamini kwamba mimi nasoma nafanya vitu vingine sina power zaidi ya kushawishi watu waniamini zaidi ya msemo wangu kwamba mimi kule nasoma, siwezi kwenda darasani nipige picha niko na madaftari no, lakini mimi nasoma niko kule kwasababu ya masomo.”
~Bongo5
Jux Awajibu Waliohoji Kwanini Hajawahi Kupost Picha yoyote Akiwa Chuo Anakosoma Nchini China
15
January 29, 2015
Tags
Kwani ni lazima awambie ama awaonyeshe pics ndio mkubali anasoma???kwani mulimuchangia pesa za kusoma ndiyo munafwatilia nyendo zake za kimasomo??? mbona munaleta ushamba kiasi hicho jameni wa tanzania....akisoma au asisome unawahusu nini nyie....kweli watu washamba....as he said darasani kwake sio kwa kupiga picha....tena musimsumbuwe huyo kijana tafadhali....it is none of your business...ama munataka kumuajiri kazi nini basi mungojeni amalize kisha wakati unamtaka akufanyie kazi basi muitishi huyo certificate.....Jamani nimemtetea tu lakini simjui msinimeze bure mie.
ReplyDeleteWe nae na ma mumumu meeeeeengi.....nenda China na ww ukasome.
ReplyDeletewhuhahahaha mdau umenifurahisha sana sidhani kama ni tanzania huyo, eti jameni... na ma mumumu yake...hahahaha niecheka sana ahsnate
DeleteHahahahaha huyo mutu balaaa muu kibaooo
Deletehasomi huyo!
ReplyDeletehasomi huyo!
ReplyDeletejamaaa umenifurahisha kuhusu ma mumumumumu ya jamaa..duh
ReplyDeleteHuyo ni muongo. Ni mwanafunzi gani anayepata muda wa kufanya kazi za kiusaniii. Atuambie ni kitu gani anachosomea. Na kama anasomea muziki hapo tutamuelewa lakini kama anasomea taaluma nyingine hapo panaweza kuwa na uwalakini. Huo muda wake wa kuzingatia hiyo taaluma nyingine anaupata wapi na huo muda wa kufanya kazi za muziki anaupata saa ngapi. Nadhani hapo kuna tatizo kubwa sana. Kuna sehemu fulani anajaribu kutudanganya. Na kama kweli ni mtu anayezingatia muda wake katika Elimu basi asingejishugulisha na hayo mambo ya muziki na hasa ukizingatia muziki wenyewe ni Bongo Flava. Kuna mtu gani ambaye hawezi kujivunia Elimu yake. Na kama ni kweli kwa nini atuwekeee huo wigo wa nini cha ku post na ni kitu gani sio cha ku post. Kwanza ni kwa nini ameenda kusoma huko Uchina?????
ReplyDeletekasome wew ndo uwe mkwel..,.......by the way Elimu yake itakusaidia nn?
DeleteKama anaweza kupiga picha za kujivunia na wanawake Malaya wa huko mitaani ni kitu gani kinachomfanya ashindwe kupiga picha ya Selfie na ya kujivunia na wanafunzi wenzake???? au japo atoke nje ya mjengo apige picha huku akiwa na vitabu vyake na pia tuone bango linaloonyesha jina la Shule anayosoma. Huyo ni muongo mkubwa haendi shule wala nini.......
ReplyDeleteUmeongea ukweli hakuna shule hapo!
DeleteMdau wa saa 5:44 am, unaonekana unapenda kujua na kufuatilia maisha ya watu wewe,,,,,,yule jamaa wa mumumumu alikwambia jux hujamchangia pesa ya kusoma so its none of your BUSINESS
ReplyDeleteNa wewe mdau hapo juu 11:13 AM unachekesha. Hebu na wewe tupigie picha na wanawake Malaya wa huko mitaani halafu itundike hapo and then tudanganye kuwa unaenda shule kule Uchina. Na pia uendeleze uongo wako kwa kutuambia kuwa wewe ni msanii..........Then hapo tutakuelewa ya kwamba is none of our business. Na pia usiache kutu tundikia grades unazozipata pale Darasani kwa kuchanganya ujinga wote huo. Unacheza wewe. Unafikiria Shule ni Mchezo mchezo. Shule na Bongo Flava ni vitu viwili tofauti. Afadhali yake Dongate ambaye yeye ameamua maisha yake yawe ya muziki na malaya wanawake kama Zari kuliko angetudanganya eti na yeye anaenda shule.......Hallooooooooooooooooooooo....
ReplyDeletehuyo atakuwa anasoma shule ya sanaa, shule kama shue ni vigumu sana kupat muda wa kuchezea kama anaopata jamaa. halafu kuhusu kupiga picha darasani wahikaji kibao wanasoma nje na wanapicha picha madarasani.
ReplyDeleteHaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa yaani nimefurahi sana kuona watu wengi wamenikomoa ati na mumu mu zangu.....bwanawe lugha kali hii na watu kama kina siss ndiyo kijijini tumezaliwa na kuzeekea hapo hapo....sasa ukivuka barabara na mie mbona utacheka mpaka ujambe...Ehhhh sasa mada yenyewe...Majemeni mbona munashindwaga kuelewa watu....nimeshasemaga hapo muache huyo kijana ,, kwani muliongeza pesa za kusoma???? hata kama anasoma corner moja karibu na choo cha munispaa.... kwani ni kitu gani!!!! nilisema hapo mwazo kwamba akirudi mtafute kisha umuandike kazi kisha utajua alichosoma huko china.....
ReplyDelete