Kaburi la Aliyezikwa na Kifaranga cha Kuku Tumboni Lafukuliwa

KABURI la Bernadetha Steven (35) aliyefariki na kudaiwa kuzikwa na kifaranga cha kuku tumboni wiki iliyopita katika mtaa wa Masekelo katika kata ya Masekelo, Manispaa ya Shinyanga, limefukuliwa na watu wasiojulikana.

Mkuu wa Upelelezi wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga, Mussa Taibu amethibitisha kuwapo kwa tukio hilo, huku akisema tukio hilo halivumiliki na kuwataka wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa wahusika wa tukio hilo.

Taarifa za kufukuliwa kwa kaburi hilo zilianza kusambaa juzi majira ya saa 1:00 usiku ambapo jana asubuhi viongozi wa eneo husika pamoja na aliyekuwa mume wa marehemu, Deo Masanja walifika eneo la tukio na kukuta kaburi limefukuliwa huku nyayo za miguu ya watu ikionekana karibu na kaburi hilo hali iliyowatia hofu kubwa.

Mjumbe wa Serikali za Mitaa wa Mtaa wa Masekelo, Josephine Kishiwa aliwaeleza waandishi wa habari kuwa alipata taarifa za tukio hilo baada ya kuelezwa na baadhi ya wananchi na kuamua kuwatafuta viongozi wenzake ili kuweza kutatua tatizo hilo.

“Tukio hili ni mara ya kwanza kutokea katika makaburi haya hatujawahi kukuta kaburi limefukuliwa, hiki kitendo kimetusikitisha tunaomba Jeshi la Polisi lifanye uchunguzi wa kina ili tujue chanzo cha tukio hili,” alisema Kishiwa.

Bernadetha alifariki dunia Juni Mosi mwaka huu na kuzikwa siku mbili baadaye ambapo wakati wa maziko yake inadaiwa ndugu wa marehemu walifanya tambiko kwa kuchana tumbo la marehemu na kuweka kifaranga cha kuku kilichochinjwa wakidai wanaondoa mikosi ili mtu mwingine asiugue ugonjwa uliomuua ndugu yao huyo, ingawa hata hivyo haikuelezwa ni ugonjwa gani.

Habari ya maziko yake ipo hapa kwenye hii thread: Shinyanga: Marehemu apasuliwa tumbo ili kuwekewa vifaranga
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mzee habari ya juni hii unasema mwaka huu?
    Kuwa makini

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad