Kina Kaka Acheni Ujinga, Hakuna Mwanamke Asiyetaka Kuhongwa! Shauri Lako

Wakaka acheni ujinga, ukitaka dem wa peke yako basi jua kugharamia. Nakwambia wanawake asilimia kubwa hukumbuka fadhila za mtu anayemgharamikia kuliko wanaume wa ai lavii yuu maneno.

Usidanganyike hakuna mwanamke asiyependa kuhongwa, kuna wanawake natural hawawezi kuomba,ila anakua anataka ujiongeze, sasa kama wewe ni wale ambao akikwambia "baby kifurushi kimekata" unajibu "basi mumy pls ukiweka nicheki" umekwishaaaa!!!

Anakueleza shida zake unasema "mpenz vumilia nakuombea upate kazi" kaka umeishaaa kabisaaaa aiseeee!!! Huna chako!!!
Ujue ulivyokata simu umefatiwa na bonge la msonyoooo ka sio tusi la nguoni basi la mwilini. Yani wewe kama ni wale wa baby mwezi huu mambo yangu hayako sawa, nakuapia unagongewa weeeeeeeeee . . . . mpaka ujute!!

Unamuona dem wako kasuka, kapendeza na hana kazi, we umekazana tu "beibi umependeza" . . . . . . Yaani wee boya ujue!! Mume mwenzio kaweka nguvu, so anapokua anatoa calendar za kukuona tulizana, service inakua kwa anayehudumia.
Hakuna dem wa siku hizi anayetaka kuambiwa nakupenda jumapili mpaka jumapili we mhonge tu uone heshima.
____________
Ujumbe wa Leo:
Old friends pass away, new friends appear. It is just like the days. An old day passes, a new day arrives. The important thing is to make it meaningful: a meaningful friend - or a meaningful day.

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Sijui kama neno kuhongwa linastahili kutumika hapo. Kama ni demu au mke wako unachofanya ni kumhudumia na sio kimhonga.Neno kuhonga linatumika pale mtu unapojaribu kufanya ushawishi wa jambo fulani kwa ajili ya manufaa yako. Kama ni demu au mke wako kimsingi huo aina ya ushawishi uliishaufanya kabla ya kuwa naye. Ndugu blogger hiyo ndio tafsiri sahihi ya hilo neno bila kupinda maana wala nini. Linapokuja suala la kutoa huduma kwa demu au mkeo ni jambo linalotegemea pale mkono wako unapoishia. Kila mtu anatoa pale mkono wake unapoishia. Na ni jukumu la wapendanao kuridhika na kile wanachokipata kutoka kwa wenzao. Pia ni lazima ikumbukwe sio kwamba ni lazima kila siku mtu atakuwa na kitu cha kutoa kama huduma. Kuna kuishiwa. Sasa kama kuna mapenzi ya dhati kati yenu basi ni lazima wote mtambue hilo na kuvumiliana mpaka pale kitakapopatika. Kina Kaka Jaribuni kuwa waangalifu sana na aina ya wanawake tegemezi. Hii ni aina ya wanawake ambao pale tu inapotokea kupunguka kidogo kwa huduma labda pengine kwa sababu za ukwasi basi ndio huyo utamsikia. Ataenda kutembeza kila sehemu ilimuradi apate kile anachotegemea kukipata. Aina hii ya wanawake ndio wanaoongoza kwa kuleta magonjwa ya zinaaa kwa wapenzi wao eti kwa kisingizio hawapati zile huduma wanazozitaka. Fungueni macho akina kaka.

    ReplyDelete
  2. Kazi ya mwanaume ndani ya nyumba ni kuudumia familia, ata kama kakosa sana awezi kukaa mwezi bila kuacha ata elf 5. utakuta mwanaume anaka na mwanamke anayo pia, ila kwakua mama ndo yupo makini na watoto, basi mwanaume uangaiki wala uulizi chochote kuhusu watoto. wanaume mubadilike, ujaacha ela nyumbani ukirudi jioni unakuta chakula na unakula unadai na kuongezewa, unajua ela imetoka wapi? utasikia wanaume wengi eti nataka mwanamke anaefanya kazi ili uwe tegemezi.

    mmh sijamaliza

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad