Lemutuz Vs Alberto Msando hii ni Vita ya Kupigania haki za Wasanii au Kopo la Coca


Kuna vita ya maneno imezuka na inayo endelea kati ya Lemutuz na Mwana sheria Albert Msando!

Hii vita ya maneno imezuka baada ya kampuni ya Coca-cola kutangaza kampeni ya kuweka majina ya watu maarufu kwenye makopo ya kinywaji cha Coca-cola na bila shaka hii vita imezuka baada ya wawili hao kushindwa kuelewana kwenye hili swala maana kila mmoja ana malengo yake!
Lemutuz ameonesha kuwa Msando ana wivu kwa kuwa jina lake halipo kwenye list ya watakao wekwa kwenye makopo huku Msando akisisitiza kuwa Wasanii wasikubali kuwekwa majina yao kama hawalipwi na akisema kukubali hilo ni kukubali unyonyaji.

Kimsingi Alberto Msando amepinga wasanii anao wasimamia kukubali kuwekwa majina yao kwenye vinywaji hivyo bila malipo yeyote yale! Na katika hili nami naungana na Msando kuwashauri wasanii wote au watu maarufu kutokubali mpango huu wa kutumika majina yao kuwatajirisha Coca-cola!

Kimsingi Coca-cola watatumia majina ya wasanii na watu maarufu kuingiza pesa huku wenye majina wakibaki watupu mifukoni! Hakika hili litatokea Tanzania pekee kama watu watakubali kutumiwa bure!

Kuna watu wako tayari kutumiwa bure lakini hawa wasanii wetu kwakweli itakuwa ni aibu sana na sitaki kuamini kama Coca-cola wana mpango wa kuwanyonya wasanii kwa njia hii huku wao wakitajirika!

Wasanii wanatakiwa kuonesha msimamo wao kwenye hili na kulipinga na wahakikishe wanalipwa ndio wakubaliane na mpango huu!

Katika hili kuna mmoja anapigania haki za wasanii na mwingine anapigania kopo la Coca-cola!
Karibuni wanajamvi

~By Ruttashobolwa/ Jamiii Forums

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. lemutuz msenge tu alafu snitchy anatumwa na watu kupumbaza wananchi pacho alivodundwa akasema kinachosemwa sio ukweli lakini asemi ukweli ni upi, bwanamdogo alivopigwa risasi nje ya maisha katokea tena na kusema sio ukweli anatumwa na watu kufanya PR hana ishu boya yule

    ReplyDelete
  2. Mm kwa kweli simwelewagi huyu Lemashuzi jamaa nimpumbavu kupita kiasi huwagasimwelewagi anashindwa hata kujua km wanamtumia yy anapenda umaarufu wakitoto hata haeundani na umriwake,stupid!

    ReplyDelete
  3. Huyu lemashuzi haoni km yy ndio mshamba,nilishangaa alivyo jigamba eti kazaliwa dar hapa ndio nikazidi kumwona urefu wa akili yake kumbe haukombali sana.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad