LULU:Mbali ya Kunizaa Kwa Uchungu, Ulizibeba Aibu Zangu...Ujumbe Mzito wa Lulu kwa Mama Yake

Lulu Michael Akiwa na Mama Yake
“Huwezi kuamini Ilinibidi nianze kuandika hii risala 3day before ur birthday (mana Sio caption tena)

Kwanza nashukuru kwa MAPENZI na heshima uliyonipa kwa kuniweka tumboni kwako miezi 9,kunizaa kwa uchungu na kunilea kiroho,kiakili na ki mwili pia...Namshukuru Mungu kwa kunipa ww kama Mzazi WANGU na ninajivunia hilo sana..!

Kuna wakati nakukosea na kukuumiza Lkn kiukweli huwa naumia na kujuta sana baada Ya kujua kosa langu.

Licha Ya uchungu uliopata kwa kunizaa na kunilea upo wakati nilipitia mambo yaliyozidi kukuumiza zaidi Ya uchungu wa kunizaa ila ktk yote ulisimama na ulizibeba Aibu zangu bila kujali jamii,familia au watu binafsi wange kuchukuliaje,Naamini wewe pekeyako ndio mtu pekee ninayeweza kusimama kwa kujiamini na Kusema ni WANGU Pekeyangu.

Una mapenzi Ya kweli,naamini Hata kama kuna wazuri wenye akili,wenye maumbo,muonekano au wenye kitu chochote kilicho bora Zaidi yangu bdo kwenye macho na Moyo wako utaniona Mimi ni bora zaidi Ya yoyote Duniani. Nakuombea Afya,Uzima,Furaha,Mafanikio na kutimizwa kwa haja zote za moyo wako.Ninakujua kama mama bora,mwanamke jasiri,mwenye msimamo,busara,hekima,mcheshi na rafiki....NENO NAKUPENDA tu halitoshi


HAPPY BIRTHDAY THE QUEEN OF MY HEART
HAPPY BIRTHDAY MAMA
Risala itaendelea nyumbani kwa Dada wa Rwechungura mana ntakesha hapa". Lulu alimaliza.

Bandiko hili ameliweka usiku wa kuamkia leo.Happy Bith Day Mama Lulu.
~Bongo Movies

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Nice massage to her mum,,,,,,,,,happy birthday mama Eliza

    ReplyDelete
  2. NIMEIPENDA MSG NZURI SANA!! I WISH TO DO TO MY MOTHER BUT!! SHE IS PASS AWAY LONG TIME!!!.
    TAKE CARE OF HER LULU!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad