Mama Abdul Awacharukia Waliosusia Kitabu Cha Kanumba

MUIGIZAJI mkongwe nchini, Salome Nonge ‘Mama Abdul’ amewacharukia mastaa wa filamu Bongo kwa kususia kujitokeza katika uzinduzi wa kitabu cha Kanumba.

Mama Abdul aliyasema hayo muda mfupi baada ya kuisha kwa uzinduzi wa kitabu hicho uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa Landmark, Ubungo Riverside ambapo alisikitishwa kutokana na marehemu kuwa mchango mkubwa katika tasnia ya filamu.

“Wasanii wetu ni wanafiki, wanapata wapi jeuri ya kumtenga Mama Kanumba wakati kwenye msiba walikuwa wote? Au tuseme wameona kwenye uzinduzi hakuna namna ya kupiga dili kama walivyozoea watawakosa watu wa kuwauzia sura.”

“Wamenikera, halafu wakimuona Mama Kanumba wanajifanya kumsalimia kinafiki. Bongo hakuna kama Kanumba waache kujishauwa,” alisema Mama Abdul.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad