KATIKA hali isiyotarajiwa, mashabiki wa Yanga waliokuwa na dukuduku la moyoni, juzi Alhamisi jioni walimfuata Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Boniface Mkwasa na kumtaka abadilishe mpangilio ili badala ya kumtumia straika Mrundi, Amissi Tambwe kuwa straika wa pili, amchezeshe akiwa straika namba moja na Mliberia, Kpah Sherman, ndiye awe straika namba mbili.
“Samahani kocha kwanza pole na kazi, tulikuwa na maoni kwamba Tambwe acheze namba tisa na Sherman acheze 10, maana tuliona katika Kombe la Mapinduzi mlikuwa mnawabadilisha sasa tumeona Tambwe anamudu sana tisa hapo tutapata mabao mengi,” alisema mmoja wa mashabiki hao huku akiungwa mkono na wenzake waliomzunguka Mkwassa kwenye Uwanja wa Boko Vetereni.
Katika kutoa ufafanuzi, Mkwasa aliwaambia kuwa hivyo ndivyo walivyopanga kuwachezesha kwa kuwabadilisha ili kuwazoesha wasikariri namba moja.
Jibu hili lilionekana kutowaridhisha mashabiki hao, lakini walimshukuru kocha huyo na kisha kumwambia tangu wameanza kukinoa kikosi hicho kimekuwa na mabadiliko makubwa na kinawapa matumaini ya kufanya vema katika mechi za Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho.
Katika hatua nyingine, beki wa Yanga ambaye pia ni nahodha, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ amemwambia kocha wa Simba, Goran Kapunovic, kuwa kazi si kuchukua Kombe la Mapinduzi, bali kushinda mechi za Ligi Kuu Bara.
“Tunaamini Yanga nzuri ingawa tulitolewa katika Kombe la Mapinduzi, mechi zile si kipimo kwamba timu yake ni nzuri. Huku kwenye ligi ndiyo sehemu ambayo Simba inatakiwa kuonyesha ubora wake,”alisema Cannavaro.
“Nimeona watu wanampongeza sana huyu kocha mpya wa Simba hata mimi nampongeza kwa ubingwa wa Mapinduzi, lakini ili watu wajue ubora wake anatakiwa ashinde mechi za ligi.”
ndio kashaanza kushinda sasa mechi ya ndanda fc
ReplyDeletewewe ni mchezaji tu kwanza una nidhamu, utaongeaje na kiongozi wewe ninani? kama yanga ni nzuri mbona hamjafunga simba mbaya, hivi yanga hamchoki kuchonga, kweli nimeamini timu yenu ni ya chama tawala, ebu bac kuweni na aibu alafu acheni kupiga kelele acha washabiki waone wenyewe. mnakera maneno mengi vitendo hakuna mdomo tu, simba mmeifunga mara ngapi? kazi visingizio tu, badala mkae mpange mikakati ili timu ifike mbele mnakalia mineno tu isiyokuwa na tija. tumechoka tunataka mpira uwanjani, hatutaki sifa za kuongea na kujinasinu kwenye vyombo vya habari
ReplyDelete