Maswali 10 kwa Vodacom Tanzania Kuhusu Shindano la Jay Millions


Maswali 10 kwa Vodacom Tanzania :Leo si siku ya 12 tangu promotion yashinda mamilioni ya jaymillionsilipoanzishwa na Vodacom Tanzania lakiniimekuwa ikilalamikiwa na watu wengikwenye mitandao ya kijamii na na mitaanikuwa "vigezo na masharti kuzingatia"inatumika kuwa hadaa wananchi. Haya nimaswali tungependa Vodacom watujibu

1. Mimi naweza leta comments 150 zafacebook na twitter zilizokuwa posted kuanzia tarehe 20-25 zikilalamikia sintofahamu ya jaymillions, je Vodacom wanaweza kuleta comments 10 tuzinazosifia?

2. Kwenye radio matangazo yenu yanasema hakuna kushiriki lakini usipotuma msg ukakatwa shilingi 300 basi huna nafasi ya kushinda, je 300 ni ya nini kama si bet ya kamari husika?

3. Je kuna tangazo lolote la redio, TV au hata bango (billboard) linalosema mwananchi atakatwa shilingi 300 kwa kila msg atakayotuma kuuliza kama kashinda?

4. Tangu shindano lianze, (ambalo mlisema mtatoa milioni 100 kila siku,milioni 10 na milioni 1) leo ni siku ya 12 ambayo kwa ahadi yenu ilibidi muwemmetoa bilioni moja milioni 400 lakini mpaka leo tarehe 26 mmetoa milioni 16 tu, je ni hizi bilioni kadhaa anapewa nani?

5. Naskia vodacom ina wateja milioni 10,wateja laki moja tu ambao ni asilimia 1 tuya wanachama wakituma msg ni shilingi 300'000'000 kwa siku sawa na shilingi 3'600'000'000 na vodacom wametoa milioni 16 tu kurudisha kwenye jamii mpaka sasa, hamuoni kua mnaondoa shilingi kwenye mzunguko na kuathiri uchumi?

6. Probability ya mshindi kutokea kwenyewatu laki moja na sio kwenye watu milioni 9 na laki 9 ni sawa na kusema kila sikuku  na nafasi moja ya pesa kuchukuliwa navodacom wana nafasi 99 za kubaki nahela, je ipo ipo siku itatokea mtu atashidamilioni 100?

7. Usiri wa kuwa mshindi atatajwa baada ya yeye kuwa katuma msg hamuoni kama inaweka mwanya wa wanaochezesha promotion kupanga matokeo nakujifaidisha wao wenyewe?

8. Je si wakati muafaka kwa Vodacom kutangazia umma kuwa promotion ya jaymillions ni kamari ambayo mshindi atachaguliwa miongoni mwa walioshiriki tukwa kutuma msg ili kuwapa wanashirikinafasi sawa ya kushinda?

9. Ni sahihi kusema jana Vodacom walikata internet kwa masaa matano wakati mjadala wa kuhoji kizungumkuti cha jaymillions umeshika kasi kwenye facebook, twitter na jamii forums?

Naamini wahusika wa Vodacom maswali haya yatawafikia, wanaweza wasijibu na hawatojibu ila kwa wanachokiona sasa kwenye mitandao ya kijamii waelewe kuwa watanzania wamebadilika,  hawapelekeshwi tena.

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. WIZI MTUPU USIMWAGE MAJI BAHARINI WALA HAITAKUSHUKURU

    ReplyDelete
  2. yan huu mtandao kero sana sio sms wanazonad ka umejshndia ayo mamilion, kwa sku sms s chn ya 20 bado za m-bet jaman

    ReplyDelete
  3. Ni kweli vodacom ni wizi mtupu.lakini kwa vile kuna akina fulani tukubali yaishe.

    ReplyDelete
  4. WIZI MTUPU JAMANI VODACOM TUACHIENI VISENT VYETU

    ReplyDelete
  5. Serikali tunaomba iingilie kati kwa sababu kwa sasa vodacom wanakata sh 300 hata kama hujaandika sms ya kurequest. Waziri wa mawasiliano tusaidie tunaumia

    ReplyDelete
  6. VODACOM KAMA NI WAJANJA BASI WAWAPOZE WATEJA WAO HATA KWA LAKI MOJA KILA MMOJA ILI KUZIMA MINUNG'UNIKO ILIYOPO,VINGINEVYO WATEJA WENGI WAMESHAWASHTUKIA.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad