Mdau Afunguka Kuhusu Wasanii na Watu Maarufu Bongo Kubebeshwa Makopo ya Coca Cola Bure

Hello Ndugu wapendwa
Nimesoma habari yenu, kuhusu na le-mutuz kuwa na ugomvi na lawyer! ni kweli namuunga mkono mwanasheria, na hii kwa kweli sio haki kwa kampuni la coca cola kuandika majina ya watu bila wao kupata chochote! (huu ni unyanyoaji wa kimacho - macho ama wazi wazi kabisaaaaa) maana mtu ama watu wanaweza kuvutiwa kununua soda only kwa sababu ya jina la mtu! sasa sielewi kama le-mutuz yeye anataka sifa tu ya kuwa kwenye makopo ya soda ama la!

mimi ni mtanzania ninaishi na kufanya kazi kati ya Namibia na Botswana, huku ni tofauti kidogo kwani kampuni ama wazalishaji wa coca cola wao mameamua kuandika majina randomly, namaanisha kuwa si majina ya watu maarufu yaani wao mameamua kuandika majina yeyote yale ya kila mtu! japo si haki!

siku ya kwanza nilibishana sana na rafiki yangu mmoja na nikamwambia hii sio haki hata mara moja kuandika majina ya watu pasipo wao kuwashirikisha kwa mwenye kampuni kujipakia kipato!! lakini huku kwa sababu watu wa huku naona hata sheria hawazijui, basi ndo hivyo tena soda zimeandikwa majina na bado zinauzwa mitaani!

kwanini ulaya hata kama mtu ama kampuni linataka kutoa jezi na kutumia jina la mtu ama mchezaji lazima waongee nae kwanza na bado lazima apewe haki miliki yake! natoa mfano kwa bia ya windhoek, drogba kashikiria windhoek bia ile, hilo tangazo  kuonekana tu vile drogba analipwa hela nyingi sana japo drogba wala sio mnywaji wa bia hiyo!

Namalizia tafadhali watanzania tusikubali kutumika!!!!!!!

Tafadhali nifichie e-mail address yangu!

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kuna Watu wametumwa hela mjini na kuna Watu wametumwa sifa mjini nakupiga picha na Watu maarufu, wote ni Watu lakini wenye mitazamo tofauti

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad