Mh. January Makamba, Urais Sio Sawa na Kucheza Filamu
4
January 19, 2015
Wanajamvini,Nawasalimu.
Nimelazimika kuanza na hiyo kauli hapo juu kutokana na unyeti wa habari yenyewe.
Nitakuwa namwendelezo wa kutoa ufafanuzi wa mambo mbalimbali yanayoikabili Tanzaniakwa kutumia mifano hai na kumbukumbu rasmi zilizopo Tanzania.
“Ni bora Simba wakali mia moja walioko Nje kuliko nyoka mdogo mmoja aliye ndani [“Godbless JonathanLema]. Haya maneno aliwahi kuyatoa Mbunge Lema, nayafananisha na kijitabualichokitoa Mh. January Makamba. Namheshimu sana [ Hata yeye anajua hilo!]lakini sina budi kusimamia ukweli na kukemea pale inapobidi!. Tanzania hii iliwahi kupata viongozi vijana wengi tu lakini historia inaonyesha waliwahi kuligarimu Taifa kutokana na ufinyu wa kufikiri na uharaka usiokuwa na tija!.Mfano Mh Raisi Kikwete, ndiye anaonekana kuwa Raisi kijana kuliko wote waliopata nafasi hiyo kwa siku za usoni lakini makubwa aliyoifanyia taifa hakuna ? aliwahi kuwa Waziri akiwa na miaka 38 tu?. Hivyo Umri sio kigezo cha kutushawishi kukupa uongozi. Uraisi sio sawa na kucheza filamu?.
Pili, Vijana tulio wengi hatuitaki ccm, yaani tunayavumilia sana majani hata hiyo rangi tungeiteketeza kabisa!!!!. Ukiona kijana yupo ccm jua lazima anapata mnofu? Vinginevyo hakuna au Baba yake aliwahi kuhudumiwa naccm hivyo na yeye anatega mpira?. Kutokana na sababu hii makini kabisa tunakuomba sana tena sana [Nakuheshimu sana Mkuu, hata wewe unajua hilo]usituharibie sifa ya ujana wetu kwa kutaka Makuu wakati bado unastahili kuwa nasubra baadae kama wataka nafasi hiyo ukaipata [ila kupitia chama kingine Mkuu].Kutunga kitabu kinachoelezea kuhusu Tanzania mpya ni maneno tu ambayo kwamtazamo wangu hayana uhalisia wowote ule.
Tatu,Nimewahi kuona watu wengi sana hasa walioko ndani yaccm wakikana maandiko yao yaliowahi kuwapa PHD, mfano DR. Harrison Mwakembe aliwahi kuzungumzia muungano wa serikali tatu kwenye kitabu chake lakini baadaye kupata tu ubunge hatimaye uwaziri kwenye uhalisia akaja kukana maandiko yake mwenyewe hivyo na hii Tanzania mpya ulioitazamia pindi utakapo pata nafasi basi itakuwa hivyo hivyo Mkuu , nakushauri egemea kwenye nini umewahi kuwafanyiaWatanzania na imebaki kama historia nasio utawafanyia nini tukikupa nafasi [uzoefu ni lulu Mkuu popote pale Duniani].Mh Nasari aliwahi kusema nanukuu ‘’CCMNI KAMA UKOO WA PANYA,BABA MWIZI MTOTO MWIZI’’ [Ukikasirika niombee].
Mwisho, Tanzania inahitaji kikongozi mwenye hofu ya Mungu [yaani mwenye hata kahistoria ka kuwa shehe,padre au hata mchungaji jamani] kutokana na sababu kuu moja kuwa Tanzania ni nchi pekee Duniani ambayo haina ‘’NationalPolicy’’ mtu akipata nafasi ya uwaziri tu anaweza kusema futa somo lahesabu kwa shule za msingi watasoma wakiwa sekondari kisa mwanae halipendi au kwasababu tu ya uswahiba na rafiki yako unaamua tu kuanzia kesho wewe utakuwa Mkuu wa wilaya [ kwa mfano tu wadau huyo jamaa alikuwa muuza chipsi leo anapata zali la kuwa mkuu wa wilaya]. Tunataka kiongozi mwenye hofu ya Mungu ili tutengeneze hizo policy kwanza maana nchi ipo pabaya.
Ila kiukweli nakupongeza kwa kutangaza nia na sio kwa kutoa kitabu, tuachie tukupime nini aulichowahi kuifanyi taifa hili Mkuu. Niombee kwa aliyekasirika. Nawatakia sikunjema
By
Elineema J Mosi
CPA[T]-Arusha,Tanzania.
Tags
Huyu jamaa kwa kweli (January Makamba) ni mtu wa kumuhurumia sana. Sijui ni kitu gani kinachomsukuma kugombea hiyo nafasi ya juu kabisa ya uongozi. Huyu bwana licha ya kwamba uwezo wake na uzoefu wake kuwa mdogo, pia matamshi yake mbalimbali yanatia shaka kama ni kweli ni mtu anayeweza kuishikilia hiyo nafasi ya juu ya uongozi. Kwa mfano aliwahi kukaririwa siku za hivi karibuni akidai kuwa Tanzania inahitaji kuwa na Kiongozi ambaye ni Dikteta. Sasa fikiria mtu kama huyu ambaye anaanza kuuwaza u-Dikteta kabla hajakamata hiyo nafasi je siku akiipata hiyo nafasi ya juu ya uongozi itakuwaje. Ni most likely ataipeleka hii Nchi katika majanga kama ilivyokuwa Rwanda ama Nchi nyingine Duniani tunavyozishuhudia majanga yanavyoendelea. Jamani tusidanganyike. Kila kiongozi ana mazuri yake na mapungufu yake. Kumshabikia January Makamba eti ataleta mabadiliko ya kimsingi sio kweli. Mabadiliko yoyote ya kimsingi katika Nchi huletwa na wananchi wenyewe. Kwani kama wananchi hawawezi kuleta mabadiliko yao wenyewe hata ashuke Masiha kuiongoza Nchi kimsingi haitawezekana. Kitu cha msingi ni kwa wananchi wenyewe kufanya maamuzi magumu ya nini wanachokitaka katika kufanya mabadiliko ya maisha yao wenyewe.
ReplyDeleteKwanza huyu bwana (January Makamba)aliwahi kwenda pale Marekani, Washington DC na kukutana na wanajumuiya ya Watanzania pale. Of course alitoa presentation moja kuhusu mstakabali wa Nchi ya Tanzania hapa ilipo na pale inapoelekea. Hili ni jambo nitakalolizungumzia hapo baadae depending na blogger atakavyoniruhusu uchangiaji wangu wa hii mada ya kukurupukia nafasi ya Urais kana kwamba ni Bongo Movie..............
ReplyDeletePumbavu we! lini vijana tulikutana na kutoa kauri moja?
ReplyDeleteHuyu Ndugu January Makamba atueleze ni kitu gani potential amefanya katika kutekeleza ilani ya uchaguzi kupitia Chama chake ambacho ni Chama tawala. Kuanzia nafasi yake ya Ubunge pale Bambuli mpaka kwenye nafasi anayoishikilia sasa ya Uwaziri wa Mawasiliano atueleze bila kutuficha ni kitu gani alichokifanya ambacho kwa kweli kina impact kwa mwananchi wa kawaida. Na pia ni muhimu atueleze msimamo wake kuhusu suala la ESCROW. Mbona amekaa kimya kuhusiana na suala hilo. Anawezaje kuziba pengo la watu masikini na matajiri hapo Tanzania. Huyu Mheshimiwa ni lazima awe na hiyo openness na transparency ili tuelewe malengo yake ni nini kuelekea uchaguzi mkuu...........Jamani Urais wa Nchi sio Bongo Movie.
ReplyDelete