LICHA ya mshambuliaji wa Yanga, Mrisho Ngassa, kuwapigia simu viongozi wake juzi Jumanne, lakini wameahidi kuendelea kumchunguza kwa kuhusishwa na kutimkia nchini Afrika Kusini kwenda kufanya majaribio ya soka la kulipwa, tofauti na alivyoomba ruhusa ya kushugulikia matatizo ya familia yake.
Wiki iliyopita Katibu wa Yanga, Jonas Tiboroha alikaririwa na Mwanaspoti kuwa alisikia Ngassa ametimkia Afrika Kusini na alipojaribu kumtafuta kwenye simu yake hakupatikana.
“Nimepigiwa simu na Ngassa usiku wa juzi Jumanne , tumezungumza mambo mbalimbali ikiwemo kumuuliza maendeleo ya matatizo ya familia yake, lakini hilo halinifanyi niache kuendelea kuchunguza ukweli juu ya tuhuma zinazoelekezwa kwake,” alisema.
Tiboroha alisema endapo kama itabainika mchezaji wao kafanya kosa hilo atawajibishwa ili iwe mfano kwa wachezaji wengine kuzingatia nidhamu ya kazi zao za kufuata utaratibu unaotakiwa na siyo kufanya mambo kiholela.