Msafara wa Waziri Muhongo wazomewa Kahama kisa fedha za Escrow

Muhongo
WAZIRI wa nishati na madini Mhe. Sospeter Muhongo amejikuta katika wakati mgumu na msafara wake baada ya kuzomewa na wananchi wa soko la wakulima katikati ya mji wa Kahama wakati akitokea kwenye ziara yake vijijini wilayani Kahama mkoani Shinyanga.
Tukio hilo limetokea hivi karibuni wakati waziri huyo na msafara wake wakitokea kata ya Bulungwa kwenye jimbo la Kahama kuelekea kata ya Bulige jimbo la Msalala kukagua ujenzi wa mradi wa umeme vijijini unaotekelezwa na wakala wa umeme vijini nchini (REA) unaoendelea kufungwa katika maeneo mbalimbali wilayani humo.
Baada ya kufika katika eneo hilo wananchi hao walianza kumzomea wakidai ni “mwizi wa fedha zilikuwa kwenye akaunti ya Tegeta Escrow kelele ambazo ziliwashtua watu wengi ambao walijitokeza kuona anayezomewa ni waziri yupi.
Hata hivyo kelele hizo ziliisha baada ya msafara wa waziri huyo ambaye yuko ziara kanda ya ziwa kutokomea na kuacha makundi mbalimbali katika eneo hilo la soko la wakulima wakijadili hatima yake katika mpango mzima wa mgogolo wa uchotwaji wa mabililioni ya shilingi kwenye akaunti hiyo ya Escrow.
Pamoja na kuzomewa na wananchi hao Muhongo katika ziara yake wilayani Kahama ameacha neema kwa wananchi wa halmashauri ya Ushetu baada ya kuwaahidi umeme katika awamu ya tatu ya mradi ya nishati vijijini.

Qoute of the Day
'You've gotta dance like there's nobody watching,
Love like you'll never be hurt,
Sing like there's nobody listening,
And live like it's heaven on earth.'
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad