Ni rafiki yake na aliyekuwa mtu wangu kwani baada ya mtu wangu kufariki kwa ajali mwishoni mwa mwaka jana amekuwa karibu sana nami, ukaribu huu haukunitia mashaka kwani kipindi bado mtu wangu yupo tulikuwa tukiambatana naye sehemu mbalimbali zikiwemo za starehe na hata kwenye shida pia.
Sasa baada ya kumaliza msiba amekuwa akinitumia pesa kidogo kidogo kwani nasoma nje ya mkoa tunaoishi hasa siku za weekend na kuniambia "mwanafunzi nenda kapate mbili tatu maana najua ulikuwa umeshazoea", na kwa sababu tumekuwa kama family friend kwa muda mrefu sikutilia shaka hata kidogo. Toka mwezi wa kumi hadi juzi ndo alikuja kikaz huku ninakosoma na ndo haya yakanikuta.
Jana akataka kinitoa out kwa kwa kuwa kwa sasa tuko kwenye maandalizi ya mitihani inayoanza jumatatu nikamtaka iwe jioni kwani muda wa mchana na asubuhi nitakuwa najiandaa kwa kujisomea, akasema na ndio utakuwa muda mzuri kwani hata yeye atakuwa ameshatoka kwenye semina pia.
Ilipofika jioni tukakubaliana tukutane kwenye resort moja hivi ambayo pia huwa kunakuwa na performance ya live band, na kweli ikawa hivyo kwa hiyo tulikula na kunywa pia. Muda wa kuondoka ulipofika dala dala zikawa zimeisha barabarani na kwa boda boda ni mbali kiasi kwamba ingeweza leta shida kwani nilikuwa nimelewa pia, tax kwa umbali ule ingekuwa ni gharama sana hivyo akanitaka niambatane naye hadi hotelin alikofikia kwan haina tatizo.
Kwa kuwa hata siku za nyuma nilishawahi kumsikia akisema kuwa yeye kama hajaamua kufanya mapenzi hawez kufanya hata kama atalala na mwanamke kwa mwezi mzima nikaamua kumwamini na isitoshe yeye ni shemeji kwa upande mwingne sikuhofia lolote.
Tukaingia kulala japo sikuvua nguo nililala na nguo zangu, sijui ilikuwaje mpaka ikawa hivyo sielewi nieleze ilikuwaje na hivi nilikuwa na pombe kidogo kichwani sielewi jamani,
Inaniuma sana kwani angenitongoza nisingemkubalia hata kidogo lakini ndo imekuwa hivyo,
nimechanganyikiwa, mke wake ni rafiki yangu sana hata sijui nifanyeje maana nikisema nimwambie nahatarisha ndoa yao, nikipiga kimya akijaga kujua itanielewaje, mwanangu na wanaye ni marafiki kiasi kwamba hata shule wanaenda kwa gari moja, nishaurini mwenzenu hata sijui nifanyeje.
Na kuhusu huyu shemeji yangu nifanyeje kwani siku zote walishasema muonja asali haonji mara moja hapa nimechanganyikiwa kiasi kwamba hata kujiandaa na mitihani tena siwezi na ndo inaanza jumatatu.Naumia sana hapa nilipo nimekosa uelekeo kuninusuru na hili janga.
Naombeni ushauri.
Poleee!!!!!!!!! Ndo ya dunia tena cha kufanya mkaushie ck akitaka kamchezo tena mtolee nje
ReplyDeletePolee!!!! Cha kufanya mkaushie ck akijileta mtolee nje
ReplyDeleteCha msingi piga kmy ck akijileta mtole uvivu
ReplyDeletePole sana na yaliyo kukuta. Tayari yalisha tokea ila nivizuri kwa kujua kwamba ulifanya kosa na unajua vizuri sababu ya we kufanya kitendo hicho sasa jitahathari sana na kitu kinacho kupeleka katika njia hiyo ili yasije yakajirudie. Kwahiyo fikiria mtihani wa kesho na achananahayo yalio tokea kwani yalitokea kwa njia ya ulevi na usijuti nahayo. Baada ya mtihani muitishe huyo shemeji kisha umwambilishe ukweli kama hutaki njia ambayo inaweza kukuletea tatizo badaae.
ReplyDeleteHuyo alikubaka. Huo ndio ukweli wa mambo. Maadam halikuwa penzi kwa utashi wako huo kimsingi ni ubakajika. Ubakaji haujalishi kama ukiwa umelewa ama la. Ubakaji ni ubakaji. Sasa basi kwa sababu tukio lenyewe limetokea kwenye Nchi ambayo wananchi wake karibia wote wana ufinyu wa mambo ya Sheria. Ndugu yangu huna chako. Hilo tena ni kovu litakalobakia katika Maisha yako yote. Na sio tu ufinyu wa kuelewa mambo ya Sheria, hata rushwa iliyokithiri bado ingekuwa tatizo kwako kupata ile haki ya kimsingi ambayo ulitakiwa uipate kwa kutendewa tendo ambalo lilikuwa nje ya utashi wako. Kitu kingine ambacho sina budi kukupa Pole Kubwa ni uelewa wako mdogo wa kutolipeleka hili suala la Aibu na udhalilishaji wa Kijinsia katika mamlaka zinazohusika. Aidha ulitakiwa uende ukaonane na wataalamu ili wakufanyie kitu kinachoitwa counselling. Lakini ni ushauri wangu tu ya kwamba bado hujachelewa, unaweza kwenda kuwaona hao wataalamu ili wakufanyie counselling na ikiwezekana na kama bado unao ushahidi wa kutosha unaweza kuliripoti hili suala polisi ili hatua za kisheria zichukue mkondo wake. Kwani ni kosa la jinai kumbaka au kutembea kimapenzi na mtu yoyote bila utashi wake na hasa huyo mtu anapokuwa mwanafunzi. Wasiwasi wangu ni kuwa siamini kama vyombo vyaSheria vinaweza kulichukulia kwa uzito unaostahili jambo hilo ilhali rushwa imetawala sana katika vyombo hivyo muhimu vya Sheria. Pole sana dada. Hizo adhari utakazozipata kutokana na tukio zima sio za kuisha leo wala kesho na kimsingi huyo jamaaa amekuharibia mstakabali wako wa maisha.
ReplyDeleteacha utoto wewe
ReplyDeleteAcha uwongo wewe mchangiaji hapo juu unataka kulikuza jambo kama huyo mtu anamakosa saaana kuliko huyo dada...!!!,hapo wote wanamakosa cha msingi kama wanaweza waombe kukutana tena ili waombane msamaha uliotoka moyoni na wasameheane kwa mambo waliyo yafanya na waishi kama zamani
ReplyDeletempe tena halafu ckilizia kama tamu usimwambie mtu, ila kama chungu kashtaki kwa mkewe
ReplyDeleteImeshatokea huna Hana ya kuchanganyikiwa ila kuwa makini
ReplyDeleteMPE tena,tatizo hajakukoleza ndo maana unajifanya kusikitika
ReplyDeletemchangiaji n0 5 hakuna kitu
ReplyDeleteukiifatilia stor vizur,huyo Dada ilpofika pale kwenye nini kiliendea baada ya kuingia ndan kavusha vusha maneno. means kwa akili ya pombe aliunga mkono process nzima kwa akili ya pombe,,ingekua ubakaji kama jamaa angekua hajalewa
lakini kwa alivyosimulia inaonyesha alionyesha ushirikiano nzur,kinachomfanya aandike hayo ni AIBU ya baada ya tendo
....hapo hakuna kuombana msamaha,kikubwa ni kuacha mawasiliano kabisa na jamaa na kama ilkua pombe na imeisha ahesabu Yale n matokeo y pombe na yamepita ""Sheria sheria" hakuna all bakwa hapo msikuze mambo na sheria zenu z kikolon
HIIIVYO