Mwigizaji Salma Jabu ‘Nisha’ na Mpenzi Wake Wamwagana

Mwigizaji wa kike  anaeonyesha uwezo mkubwa  kwenye tansia ya  filamu hapa Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’  na mpenzi wake aliyejulikana kwa jina la Farhad wanadaiwa kumwagana baada ya kuwa kwenye uhusiano kwa muda mrefu.

Chanzo makini cha GPL,kilisema kwamba Nisha na mpenzi wake huyo ambaye walikuwa na mipango ya kuoana mwaka jana lakini ndoa ikayeyuka waliachana kutokana na sababu zisizojulikana na sasa kila mmoja  yupo bize na maisha yake.

Baada ya kuzinyaka habari hizo paparazi GPL alimtafuta Nisha ili kuzungumzia habari hizo ambapo alikiri kwamba ni kweli wamemwagana.“Sababu za kuachana siwezi kuziweka wazi kwa sasa, niko kikazi zaidi mambo ya mapenzi nimeyaweka pembeni nataka nitimize malengo yangu ambayo hayakutimia mwaka jana,” alisema Nisha.

Nisha alifunga mwaka 2014 kwakuingiza sokoni filamu yake ya HAKUNA MATATA ambayo inafanya vyema sokoni hivi sasa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad