Mwanasheria Albert Msando Amlipua Mwigulu Nchemba na Kashifa ya Kudanganya Umri

Siku chache baada ya Mwigulu Nchemba kupewa barua ya kumtaka ache ziara zake ,sasa wabaya wake wamejitokeza na kuleta visibitisho vinavyo onyesha Mwigulu amezaliwa miaka miwili tofauti. Wakati cheti chake cha masters kinaonyesha amezaliwa 1978 ,cheti cha form four kinaonyesha huyu jamaa amezaliwa 1975 Mwigulu njoo hapa utuambie ulizawaje miaka miwili tofauti. .. Source wall page IG by Alberto msando.


"Hii nchi tatizo la miaka ni sugu. Kila mtu ana umri wake. Kaka yangu Mwigulu Nchemba alizaliwa Mwaka 1975 na 1978 kwa mujibu wa vyeti vyake vya elimu. Alianza Form One Ilboru akiwa na miaka 19. Ingawaje Transcript ya Masters inaonyesha alizaliwa Mwaka 1978. Na sasa ni Mchumi, Kiongozi wa Chama, Mbunge na Naibu wa Waziri wa Fedha. Nadhani ni muda muafaka suala la taarifa sahihi za umri likafanyiwa kazi. La sivyo kila wakati litajitokeza kama kashfa kwa wahusika. Hatujui nani kafikisha umri wa kustaafu na ana umri wa kupiga kura nk. Ila kila kitu kinawezekana. Hii ni Tanzani nchi ya ASALI na MAZIWA. #TwendeKazi #NaaminiAnajuaKuhesabu #UmriTena" Alberto Msando



Tags

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Dah haya bwana!!!!

    ReplyDelete
  2. sasa msando naye kaanza kutafuta kick za kifala

    ReplyDelete
  3. HAYA TENA MWINGULU TUWEKA WAZI 75 AU 78??????????????

    ReplyDelete
  4. wala sio kick hapa tunataka ukweli kunya anye kuku akinya bata kaharisha!!!!!

    ReplyDelete
  5. Sasa kama Kiongozi mwenye hadhi kama yake anashindwa kuwa mkweli kwa jambo kama la umri, itakuwaje kwa vitu vingine na vya maana kwa Taifa na Wananchi kwa ujumla??? Nadhani Mwigilu Nchemba anafahamu hiki kitu vizuri na kama kulikuwa na makosa ya uchapaji basi angesimamia na kuhakikisha makosa yanarekebishwa kuliko kuruhusu utumbo kama huu kuwekwa hadharani kama kashfa...............Mwigilu Nchemba tunategemea utatujibu majibu ya kuridhisha juu ya udanganyifu ulioufanya wa umri wako.

    ReplyDelete
  6. Tatizo la huyu jamaa hata jina analotumia si jina lake halisi.Jina Mwigulu Nchemba ni jina la kijana mmoja wa kisukuma aliyefaulu darasa la saba,lakini kama tujuavyo jamii za wafugaji hakwenda sekondari,nafasi yake ikauzwa kwa mbuzi mbili kwa huyu anayejiita Mwigullu Nchemba sasa.Kwa wanyeramba hakuna ma jina kama hayo.Hata umri wake amechakachua pia.Ni Tanzania ya ccm tu unaweza kufanya uhalifu kama huo ukaendelea kutamba mtaani na kulundikiwa vyeo.Majanga!!

    ReplyDelete
  7. Ilisemwa 'if you live in glass house do not throw stones'Mwigullu ulifurahia kykashifu na scandalize wenzio sasa zamu yako imefika.

    ReplyDelete
  8. Mwigilu Nchemba acha kutudanganya. Hiyo Mikutano yoote unayoifanya huko Mikoani ni gelesha toto. Unachofanya ni kuwadanganya wananchi walio maskini na kufunika ule uozo wa suala la ESCROW ambalo kimsingi Chama Tawala (CCM) mmeshindwa kulichukulia maamuzi magumu.Sasa mnabakia kulindana kwa kwenda mikoani na kuwadanganya wananchi walio maskini na ambao hawaelewi chochote.

    ReplyDelete
  9. Mwachen Mwigulu aendelee na movement zake msimfualltilie kwa kumuharibia hili ni jambo ndg wakil ungemuuliza angekupa jibu. Nataman Mwigulu awe Rais ajae

    ReplyDelete
  10. Tanzania hii kila mtu anatafuta kuandikwa na magazeti mitandao ndo raha yake duuh bongo bana

    ReplyDelete
  11. chezea wabongo weye

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad