" Natamani Kwenye Amri za Mungu Iongezwe ya 11 Isemayo 'USIWE CCM'.."....Hii ni kauli ya Lema Bungeni

LEO Wabunge wameendelea kuchangia taarifa za Kamati za Hesabu za Serikali PAC na LAAC zinazoonesha ubadhirifu mkubwa wa fedha za umma. Hapa  chini nimekuwekea  michango  ya  baadhi  ya  Wabunge.


Lema: Haiwezekani kila siku tukija humu tunazungumzia wizi tu, inatakiwa tuzungumzie mipango ya maendeleo ya wananchi sio kila siku wizi wizi wizi unaosababishwa na CCM.

Lema: Kama ningeweza kupendekeza pia kwenye Amri Kumi za Mungu, ningependekeza iongezwe amri ya 11 inayosema 'USIWE CCM'

Lema: Katika mazingira kama haya, nathubutu kusema 'My Country is like a Getho' mambo hayaendeshwi kwa utaratibu kabisa

Esther Bulaya: "Yani watu wanagawana posho Bilion 9, na wanafunzi wanasoma kwa shida halafu mnataka tuwapigie makofi haiwezekani"

Esther Bulaya: "Hatuwezi kila siku tunakuja hapa majibu yaleyale kila siku wizi wizi wizi, haiwezekani, hawa watu washughulikiwe"

Lissu: "Kinachotufikisha hapa ni Rais kushindwa kutimiza wajibu wake wa kikatiba wa kuwawajibisha watendaji wake"

Lissu: "Tunachotakiwa kufanya hapa ni kuanza na hawa mawaziri tulionao humu ndani, tukubaliane kuwawajibisha"
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Esther wewe mwanamke wa shoka nakukubali kwa 100% nakuombea uje kuwa rais wa nchi hii. wewe unasema kweli daima wewe mchapa kazi sana wewe ni mzalendo wa kweli

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad