Wizara ya Fedha imesema hatua za awali zilizoanza kuchukuliwa na Rais Jakaya Kikwete kushughulikia maazimio ya Bunge kuhusu sakata la uchotwaji fedha zaidi ya Sh. bilioni 300 katika akaunti ya Tegeta Escrow zimewezesha wahisani kuanza kutoa misaada waliyokuwa wamesitisha.
Naibu Waziri wa wizara hiyo, Mwigulu Nchemba, alisema hayo jana wakati akihojiwa katika kipindi cha Kumepambazuka kinachorushwa na Radio One.
Nchemba alisema katika nusu ya mwaka wa kalenda wa fedha kulikuwa na changamoto nyingi ikiwamo wahisani kusitisha misaada yao kwa Tanzania kusubiri maamuzi yaliyotolewa na Bunge kuhusiana na sakata la Tegeta Escrow.
Alisema uamuzi uliochukuliwa na wahisani kusitisha misaada kwa Tanzania kwa muda ni fundisho kwamba kama nchi tunahitaji kuwa na matumizi mazuri ya fedha na kuwa na kujenga misingi ya kujitegemea. “Kama Taifa tuanze misingi ya kujitegemea, tumepata fundisho kupanga miradi ya maendeleo halafu unategemea fedha za wahisani ni tatizo,” alisema.
Nchemba alisema kutegemea wahisani ni tatizo ambalo nchi inabidi kujipanga kuondokana nalo kwani hali hiyo inakwamisha miradi kuchelewa kutekelezwa wahisani wanaposhindwa kuleta fedha kwa wakati.
Wahisani wanaosaidia bajeti ya Tanzania ni pamoja na African Development Bank (AfDB), Canada, Denmark, Umoja wa Ulaya, Finland, Germany, Ireland, Japan, Norway, Sweden, Uingereza na Benki ya Dunia. Benki ya Dunia na wahisani wengine kwa muda sasa wamekuwa wakisaidia katika miradi mingi ya ujenzi yenye thamani ya zaidi ya Dola za Marekani milioni 230.
Mwishoni mwa mwaka jana, Marekani ilibainisha kuwa mkataba wa pili wa miradi inayofadhiliwa na shirika lake la Changamoto za Milenia (MCC) utategemea hatua zitakazochukuliwa na serikali ya Tanzania dhidi ya wahusika wa kashfa hiyo.
Taarifa iliyotolewa na Desemba mwaka jana na ubalozi wa Marekani nchini ilieleza kuwa wakurugenzi wa MCC waliokutana katika mkutano wao uliofanyika Desemba 10, mwaka huu wamesikitishwa na hali ya rushwa nchini Tanzania.
CHANZO: NIPASHE
Hakuna hatua zozote za maana ambazo zimechukuliwa zaidi ya gelesha bwege. Hao waliotakiwa kujiuzulu au kufukuzwa kazi imekuwa mbinde kuwang'oa, huyo Waziri wa Nishati bado wanamlindalinda. Kimsingi Uongozi wa Nchi umeoza. Na ninashangaaa hao wahisani wanairudisha kivipi hiyo misaada. Ilitakiwa ifutwe kabisaaaaa.
ReplyDeleteHakuna hatua zozote za maana ambazo zimechukuliwa zaidi ya gelesha bwege. Hao waliotakiwa kujiuzulu au kufukuzwa kazi imekuwa mbinde kuwang'oa, huyo Waziri wa Nishati bado wanamlindalinda. Kimsingi Uongozi wa Nchi umeoza. Na ninashangaaa hao wahisani wanairudisha kivipi hiyo misaada. Ilitakiwa ifutwe kabisaaaaa.
ReplyDeletecjui tutategema hawa wahisani mpaka lini? ndo maana tunanyonywa tu na hawa watu.
ReplyDelete