Nyalandu Aanza Kampeni Kanisani, Amhusisha JK na Majini

Jana kwenye ibada ya mkesha wa kuupokea mwaka mpya uliooneshwa live star TV, Waziri Nyalandu alijitokeza wazi na kuongea kikampeni akiomba waumini wa dini ya Efata kumchagua kuwa Rais.

Isitoshe, Nyalandu aliongelea utawala wa Rais Kikwete kuwa ni utawala unaolindwa na majini saba, ingawa hakufafanua alimaanisha nini, lakini alishangiliwa sana na waumini wa Efata.

Anayejiita nabii na mtume Mwingira, naye aliongeza kuonesha wazi kuwa Nyalandu ndie chaguo lao.

My take: Huo ni udini wa wazi kabisa. Nyalandu ameanza kutumia kanisa analosali kuomba kura za waumini wake.

Kuna maneno ambayo yamemkosea adabu Mwenyekiti wa CCM, Professa Kikwete, kwamba analindwa na majini saba. Sina hakika kama maneno hayo ni rasmi ndani ya CCM au ni ya kanisa la Mwingira.

Wadau karibuni.

Source: Star TV live broadcast Mkesha wa mwaka mpya.
~Credits:Jamii Forums

Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. HAFAIIIII!!!!!!!

    ReplyDelete
  2. TANZANIA ITAENDELEA KUWA NA MICHOSHO TU KAMA VIONGOZI WENYEWEWE KAMA HAWA, AMWAGE SERA ZA NINI? ZA UONGO, NA UFISADI

    ReplyDelete
  3. viongozi wanaongiza dini na siasa ni hatari kwa Taifa, tena ni wa kumuogopa kama ukoma, in short huyu baba au kaka Hafaiiii

    ReplyDelete
  4. Mpuuzi tu akitaka kuwa rais labda awe rais wa hilo kanisa lao la kishetani aka Freemason

    ReplyDelete
    Replies
    1. usisema kitu ambacho huna hakika nacho tafadhali. Kanisa la mungu. japo alichofanya kanisani sio sahihi!!

      Delete
  5. Mlokole mwenye kupenda totoz, hivi alisahau iliandikwa uzisini? Hakuna wokovu pasina matendo ya haki na kweli. Kwenye ujangili yumo, kwenye kugawa vitalu katika hali ya sintofahamu yumo. Haya na yeye atalindwa na mashetani wangapi?

    CCM mchagueni huyo mpate anguko kuu, hata akipigiwa kampeni na nani watu tunamjua siku nyingi Nyalandu amejawa na chuki za kidini. Kiufupi ni mbaguzi wa watu kulingana na dini zao, na Mungu kamuumbuaje?

    Na hilo kanisa aliloenda nalo ni la vituko kweli, wakati JK amechaguliwa awamu ya 1, walifunga na kusali siku 7 ili JK afe, waumini wakawa wanatoa ushuhuda wanasubiria afe, wamesubiri wee mpaka mwaka huu anatimiza vipindi vyake 2. Hivi wewe Mwingira unafikiri Mungu huwa anapokea maombi ya chuki za kijinga kijinga? Ndio maana umebaki kuwadanganya waumini wako eti JK analindwa na majini 7. Uliyaonaje kama na wewe sio jini? Hahahahaaa wewe kula pesa ya sadaka ponda raha achana na kusambaza ujinga.

    ReplyDelete
  6. hili jamaa bwege kweli, hata sijui lilikuwa linaongea nini? eti ndiyo aje kuwa raisi wa Tanzania, labda apigiwe kura na watu waliokufa!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad