Kutokana na tukio hilo, Jeshi la Polisi liko katika msako mkali, huku Mkuu wa jeshi hilo, IGP, Ernest Mangu akitangaza donge nono la Sh milioni 20 kwa watakaofanikisha kukamatwa kwa wahusika wa tukio hilo na silaha.
Akizungumza na waandishi wa habari kwa njia ya simu kutoka eneo la tukio, Ikwiriri, Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Ulrich Matei alisema majambazi hao walitumia silaha kuwaua askari hao.
Kamanda Matei alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 8 usiku katika kituo hicho cha Polisi cha Ikwiriri. Aliwataja askari waliokufa kuwa ni mwenye namba E 8732 Koplo Edgar Milinga na WP 5558 Konstebo Judith Timothy.
Alisema licha ya kufanya mauaji hayo, pia majambazi hayo yalipora silaha tano za moto aina mbalimbali, zikiwemo SMG 2, SAR 3 na risasi 60. Pia, walichukua mabomu mawili ya machozi.
Kamanda alisema kuwa pia watu hao, waliharibu kwa kulipiga risasi gari la Polisi la kituo hicho lenye namba za usajili PT 1965.
Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Advera Bulimba alisema tukio hilo la kusikitisha, halitapita hivi hivi, bali jeshi limeelekeza nguvu zake huko kuhakikisha wahusika wanakamatwa.
Alisema tayari Mkuu wa Jeshi ametangaza dau la Sh milioni 20. Pia, alisema katika kuongeza kasi ya msako, Kamishna wa Operesheni na Mafunzo, Paul Chagonja akiwa na timu ya makachero, yuko eneo la tukio kuhakikisha wahusika, kokote waliko, wanasakwa na kutiwa mbaroni.
“Hili ni sawa na tukio la kigaidi, Jeshi la Polisi litakabiliana na wahusika kokote waliko, lazima wakamatwe. Kikubwa tunaomba ushirikiano wa wananchi, tunaamini wengi ni raia wema na watalisaidia jeshi kufanikisha jukumu hilo la kukomesha uhalifu nchini,” alisema Advera.
Aliwataka wananchi kuelewa Jeshi la Polisi liko imara, hivyo wasiwe na hofu yoyote juu ya tukio hilo. Alisisitiza kuwa wahusika wote watadhibitiwa na kushikishwa adabu
Quote of The Day:
When you wake up every day, you have two choices. You can either be positive or negative; an optimist or a pessimist. I choose to be an optimist. It's all a matter of perspective.
poleni sana familia za marehemu Mungu azipumzishe roho zao mahli pema peponi, lakini nikija upande wa Askari ambao bado Mwenyezi Mungu amewapa pumnzi hebu jaribuni kutunza siri za jeshi kama askari wa zamani na kama mlivyoapa kwa ajili ya kazi hiyo. tatizo kubwa limekuwa ni kwamba askari mmekua ndio vinara wa kutoa taarifa kwa watu wanaoshukiwa kwa uharifu kwa ajili ya hongo mnazopewa hivyo mnatuvunja moyo wanannchi wazalendo na kutufanya tuhofu kutoa taarifakwa kuhofia roho zetu, tena mnafanya hivyo bila kujua kwamba kwa kutoa siri za jeshi mnajikaanga kwa mafuta yenu wenyewe, kwenu askari wote TUNZENI SIRI ZA JESHI ILI WANANCHI WAWAPE TAARIFA ZA WAHARIFU na washughulikiwe kwa ufasaha. nasisitiza tutawapa ushirikiano .
ReplyDeletePolenisana askari wetu,ila mbona mkuu mangu havumi kama alivyokua saidi mwema? au uhalifu uumepunguasana,tulishazoea kilasiku mitandaoni magazeti yote nimwema vipi au uhalifu naona kimya
ReplyDelete