Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari mauaji hayo ya kikatili na kutisha yalitokea juzi saa 5.30 usiku nyumbani kwa marehemu.
Kidavashari alisema, siku hiyo ya tukio marehemu alikuwa amelala nyumbani kwake akiwa na mkewe Meklina Mussa na ghafla walitokea watu watano ambao hawafahamiki na kuvunja mlango na kuingia ndani ya nyumba.
Alisema baada ya mkewe kujifunika walianza kumchinja marehemu kwa kutumia panga huku mkewe akiwa anasikia jinsi marehemu akilia kwa uchungu.
Kidavashari alisema baada ya kumchinja walichukua kichwa na kukiweka kwenye safuria na maji na kukipika kwenye moto uliokuwa unawaka nje ya nyumba ya marehemu.
Alisema kisha walirudi ndani na kunyofoa sehemu za siri, mikono na miguu na kuziweka kwenye safuria jingine kwenye moto na kutokomea kusikojulikana huku viungo hivyo vikiendelea kuchemka ndani ya safuria hizo.
Kuna ki2 c bure!!!!!!!
ReplyDeleteKuna ki2 c bure
ReplyDeleteJaman mbona inasikitisha
ReplyDeleteinasikitisha kweli!!!!!!!!!!!!
ReplyDeleteMbona inasikitisha
ReplyDeleteNi mambo ya Siasa au kuna lingine? Maan km n siasa bora uwe huna chama kwa hali hiyoo, Pole kwa family yake
ReplyDeleteEEE MWENYENZI MUNGU TUEPUSHE NA UKATILI HUU WA KUTISHA
ReplyDelete