Mkongwe wa muziki wa hip hop Afande Sele, amekiri kuwa tayari kwa upande wake siasa imekwishaanza kumpunguzia kasi katika kufanya muziki, huku akiwaomba radhi mashabiki wake kumvumilia kidogo kabla ya kumsikia tena akitoka na rekodi mpya.
Afande Sele amesema kuwa, sanaa ya muziki ambayo kwake anaichukulia kama mke mkubwa, imeifungua milango kwa mke mdogo ambaye ni siasa, katika mwaka huu wenye harakati nyingi zaidi, ujio wake mpya kisanaa ukitarajiwa kuanzia mwishoni mwa mwezi wa pili.