Ujumbe Toka Kanda ya Ziwa kwa Wanaume wa Dar es salaam Walioshindwa Kupigana na Panya Road

Wanaume wa dar kweli mmedhihirisha ni waoga wa kutupa. Ijumaa nyinyi wenyewe ndo mlikuwa vinara wa kutangaza hofu kuwa kuna panya-road, 
Alafu ndo wenyewe mlikuwa mstari wa mbele kufunga maduka na kukimbia hovyo hovyo hata hao panya hamjawaona. 

Ni aibu sana hii kwa mwanaume. Yaani badala ya kuhamasisha wanaume wenzenu mjitokeze kupambana na panyaroad, nyie ndio mnahamasisha watu wafunge biashara wakimbie! 

dah aibu kweli hii. Ulegevu huu huwezi kuukuta huku Kanda ya Ziwa maana kwenye dharula kama hiyo huwa kuna vitu vifuatavyo wanaume mlipashwa kufanya:

Kupiga yowe na kukusanyika kwenda kuwafyekelea mbali hao panya Road. 

Sasa basi ili muwe majasiri inabidi muache mambo ya kitoto kama:

Kunywa kahawa na kashata na joto lote lile.

Achaneni na kula pweza kuleni ugali wa mhogo na sangara.

Vitu kama ngisi, kachori na juice ya miwa vinawafanya muwe nare nare sana.

 Ni aibu kwa mwanaume kuweka chumvi pilipili na ndimu kwenye mahindi ya kuchoma au
kuweka chumvi kwenye embe.

 Acheni mara moja kula ubuyu mnajidharirisha mno.

 Komeni kuangalia tamthiliya kwenye Haya ndio baadhi ya mambo yanawafanya muwe mdebwedo wa kutupa. Mkiendelea hivi ipo Siku panya road watakuja kuomba wawekewe maji ya kuoga na wake zenu mchana kweupe na nyie mpo. Jiangalieni sana...

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kweli Kabisa wanaume wa dar Kazi kukaa vibarazani kupiga umbea!!!!! Na Malaya

    ReplyDelete
  2. YAANI MI NI MWANAMKE NA NILIKUWAPO UBUNGO, JAMANI NI AIBU WANAUME NDO WANATUPIGA VIKUMBO KUKIMBIA BADALA WAJIKUSANYE KUPAMBANA,NI JIJI AMBALO KINA MAMA INABIDI TUENDEGE GEAM TU!
    UKISEMA WANAUME WAPO UTAKUFAAAAAAAA

    JAMANI KINA BABA ONENI HIYO AIBU ILIYOWAKUTA MPANGE MIKAKATI MJIREKEBISHEEEEEEE,WANAUME KOKOTE NDO TEGEMEZI ILA KWA DAR NI SHEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEDA

    ReplyDelete
  3. UKWELI WATOTO NA VIJANA WANALELEWA KATIKA MAZINGIRA MAGUMU SANA. TUNAIOMBA SERIKALI NA TAASISI BINAFSI KUONGEZA NAFASI ZA AJIRA KWA VIJANA HASA KATIKA KILIMO, VIWANDA, NA MASOKO KWA BIDHAA NA FANI MBALI MBALI ZA VIJANA NDIPO TUTAWEZA KUPUNGUZA WALAU KWA UCHACHE TATIZO KAMA HILI LA PANYA ROAD. MUNGU IBARIKI TANZANIA MUNGU IBARIKI AFRIKA. KP the don

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad