Mambo yanayotokea kwenye kutangaza na kuapisha washidi Wa uchaguzi Wa serikali za mitaa ni dalili mbaya ya kitakachotokea kwenye uchaguzi Wa urais Wa 2015 Kama UKAWA watashinda 2015.
Ukawa itashindwa tu 2015 Kama wasimamizi, wanaotangaza na kuapisha mshindi wataendelea kuteuliwa na kupokea na kutii maagizo na amri kutoka kwa wakuu wa wilaya, wakurugenzi Wa wilaya, wakuu wa mikoa na Rais Wa nchi.
Kama utaratibu utaendelea kuwa Kama ulivyo Sasa wapinzani ni bora kuanza kujiandaa kushindwa tu Tena 2015.
Vinginevyo hamna budi kuanza Leo kutafakari namna wasimami, watangazaji Wa matokeo na waapishaji Wa walioshinda watakavyokuwa huru uchaguzi Wa 2015.
Au muwe na cha kufanya Kama atatangazwa na kuapishwa yule ambae hakushinda Kama ilivyotokea kwa Mwai Kibaki kule Kenya.