Warioba Azungumzia Tetesi za yeye Kuhamia Ukawa na Kuwania Uraisi 2015

Jaji Joseph Warioba
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba, amesema kamwe hawazi kugombea urais wala kurudi kwenye harakati za siasa na wala hana mpango wa kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Akizungumza na NIPASHE katika mahojiano maalum jijini Dar es Salaam jana, Jaji Warioba alisema kuna ‘wakubwa’ fulani wanaoendesha kampeni ya kumkejeli na kumkashifu; huku wakizusha kwamba ana mpango wa kuhamia Upinzani; tuhuma ambazo alisema siyo za kweli.

“Miezi michache iliyopita, kulikuwa na habari zinazunguka kwa wakubwa fulani zikisema nimejiandaa kuhama CCM kwenda Ukawa. Nikaona ni katika mtindo ule ule wa kutaka kuchafua jina langu,” alisema.

Alisema: “Mwanzo, wakubwa hao walimchafua kwa kudai kuwa amemsaliti Mwalimu Julius Nyerere na sasa wamekuja na hoja kwamba anataka kwenda Ukawa na kufikia hatua ya kutaja hadi siku atakayotangaza kuhamia Ukawa jambo ambalo halikutokea.”

Alisema watu wanaoibua tuhuma hizo ndio wamekuwa wakimtukana, wakimkebehi na kumkejeli.

Alisema mwaka 1995 aling’atuka kwenye utumishi wa umma na mwaka 2002 aling’atuka kwenye uongozi wa chama ambako alikuwa kwenye vikao vya chama kwa takribani miaka 26.

“Na baada ya hapo sina hata wazo la kusema tena nirudi ama kwenye utumishi wa umma ama kwenye siasa, wanaosema hivyo wanaejenda yao. Yote haya yanayosemwa hanaya msingi, hakuna njia ambayo mimi ninaweza kurudi tena,” alisema.

Alisema hata kama angetaka kurudi kwenye siasa asingekwenda Ukawa bali angefuata taratibu za chama chake.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad