Yaliyojiri Bungeni: Vurugu Zaibuka BUNGENI Kuhusu LIPUMBA Kupigwa na Polisi Jana
3
January 28, 2015
Mbatia alisimama na kutoa hoja ya dharura ijadiliwe Bungeni kuhusu Polisi Dar es Salaam kutumia nguvu dhidi ya wanachama wa CUF na kuwapiga.
Mbatia: "Nimesikitishwa sana, Lipumba amepigwa, watoto wamepigwa, waandishi wa habari wamepigwa, na Polisi wakasema wamepewa maagizo"
Mbatia: "Prof Lipumba ni Mwenyekiti wa chama chenye wabunge zaidi ya 30 na Mwenyekiti wa chama kinachoshiriki serikali ya Zanzibar, sasa kama yeye anafanyiwa hivi itakuwaje Wananchi wa kawaida?"
Mbatia: "Naomba kutoa hoja Bunge liahirishe shughuli zake ili tujadili tatizo hili lililotokea"
Lakini Spika Anna Makinda aliipinga hoja yake na kusema,
Spika Makinda: "Naiagiza serikali iandae taarifa kamili, kesho ilete humu Bungeni, ndipo nitaruhusu hoja hii ijadiliwe, Sasa Hapana".
Spika Makinda: "Someni kanuni vizuri, zinaniruhusu kuamua kama kadri ninavyoona, hoja za namna hii haziungwi mkono"
Hilo likazua tatizo baada ya Baadhi ya wabunge wengi wa upinzani kugoma kuendelea na ratiba, wanataka ijadiliwe sasa, wanapiga kelele, kuna hali ya taharuki.
Spika Makinda akaamua kusitisha shughuli za Bunge hadi saa 10:00 jioni kutoa nafasi ya makubaliano kuhusiana na suala hilo
Tags
POLICE WAMETUMIA NGUVU MNO KUPITA MAELEZO!! SIO FAIR KABISA
ReplyDeleteheshima ya utanzania wetu lazima izingatiwe kwa wenyeviti wote wakati wowote wenyeviti wa vyama vyote wapewe heshima wakati wakikamatwa kwa kuvunja sheria sio waadhirishwe km mbogo haipendezi kwa nchi km yetu mbele ya raia na jamii zengine
ReplyDeleteTusilazimishe Jeshi la polisi lifanye kazi kisiasa ndoa sababu vituo vya polisi vinavamiwa mapolisi wanauawa hakuna anayelaani wapolisi
ReplyDelete