Zitto Aishukia EWURA Juu ya Kutoshuka kwa Bei ya Mafuta Tanzania
4
January 05, 2015
Kuanzia Mwezi Julai mwaka 2014 mpaka Desemba, bei ya mafuta ghafi imekuwa ikishuka kutoka $110 kwa pipa mpaka $56 kwa pipa.
Mporomoko huu wa bei wa zaidi ya 40% haujaleta unafuu kwa mtumiaji wa kawaida wa mafuta wakiwemo wenye daladala, mabasi wala taxi na kupelekea nauli za usafiri wa umma kupungua. Leo bado bei ya mafuta kwenye vituo vya mafuta ni tshs 2029 kwa Petroli na 1909 kwa dizeli, bei ambayo ni karibia ile ile kwa miezi michache iliyopita.
EWURA, inasemekana wamesema kuwa bei za hapa nchini hushuka baada ya miezi 2 kwa sababu waagizaji huagiza kwa ujumla mafuta mengi zaidi na hivyo kutofaidika na punguzo la bei. Hata hivyo bei zimeanza kushuka toka mwezi Julai na hatujashuhudia unafuu wowote kwa wananchi.
Kinachosikitisha ni kuwa, ingekuwa bei ya mafuta imepanda tungeona bei zimepanda mara moja na sababu za kununua 'bulky hazingetolewa kwetu na Mamlaka husika.
Ni kweli kwamba Tanzania hununua mafuta yaliyosafishwa na hivyo bei inayoshuka sio hiyo. Lakini hao wasafishaji hununua mafuta ghafi yenye bei ndogo hivi sasa kwa hiyo ni dhahiri lazima bei za pampu zipungue.
Vile vile ni kweli kwamba thamani ya shilingi ya Tanzania imeporomoka hivyo wananchi hawawezi kuona unafuu wa bei ya mafuta kwa sababu hununuliwa kwa fedha za kigeni na kuuzwa kwa Sarafu yetu.
Hata hivyo, kasi ya kushuka kwa bei ya mafuta ni 40% wakati shilingi imeshuka kwa chini ya 10%. Katika hali ya kawaida na kwa kutumia mfumo wa kukokotoa bei wa EWURA, angalau bei ya mafuta ingeshuka kwa kati ya 15% and 25%.
Ni dhahiri mamlaka za nchi na hasa EWURA wanapaswa kuueleza umma ni kwanini bei za mafuta hazishuki kulingana na bei ya bidhaa hiyo katika soko la Dunia bila kutumia visingizio visivyo sahihi. Wananchi wana haki ya kujua na kama hakuna Maelezo basi bei hizo zishuke na wananchi wafaidike na punguzo hilo.
Chanzo: Fikra Pevu
Tags
YAANI HII TANZANIA INASHANGAZA KWELI, UTAFIKIRI HATUNA MFUMO WA AINA YOYOTE KATIKA KUJIONGOZA, MAFUTA YAMESHUKA KARIBU DUNIANI KOTE
ReplyDeleteDah!! Kwa kweli ni aibu sana. Hili suala lilikuwa sio lazima lizungumzwe na wana siasa kama Zitto. Wataalamu wa Uchumi pekeee wangetosha kulizungumzia na kurekebisha gharama za mafuta ili kuleta unafuu kwa watumiaji. Lakini mpaka inafikia hatua ya wanasiasa kuingilia kati kwa kweli shughuli ipo. Hilo Taifa la Tanzania lina safari ndefu sana ya kufika huko tunapopataka.
ReplyDeleteKUNA WATALAAMU WA UCHUMI TANZANIA NA AFRICA KIUJUMLA, HMMM SI KUNGEKUWA NA MAENDELEO YA MABADILIKO YA KILA NYANJA, HAKUNAAAA, BALI KUNA WATALAM WA KUCHAKACHUA NA UFISADI WA MATAIFA YAO, NDIO MAANA KILA SIKU KUKO ZIIIIII, DACK CONTINENT
ReplyDeleteKusema ukweli Serikali yoyote makini ingeingilia kati na kufanya marekebisho ya being ya mafuta ili kuleta unafuu kwa wananchi ambao wengi wao no maskini. Hili suala la mafuta lingesaidia kushusha mfumuko wa bei za bidhaa mbalimbali na kumsaidia mwananchi wa kawaida katika mahitaji ya kila siku.Serikali yetu haina huruma kabisa.
ReplyDelete