“Napenda kusema kuwa mimi ni mbunge halali wa Vunjo na Mbatia hatapata jimbo hilo na ninatangaza kuwa nitagombea tena na hafi mtu hapa“– Alisema Mrema wakati akimalizia kuwasilisha hoja yake hiyo.
Jana wakati wa kikao cha Bunge jioni, Mbunge Mbatia alipata nafasi ya kujibu kuhusu ishu hiyo:
“Maelezo haya nayatoa kukanusha kwa moyo wangu wote matamshi yaliyotolewa ndani ya Bunge hili na Mheshimiwa Augustine Lyatonga Mrema, Mbunge wa Vunjo.
"Siku ya tarehe 05/02/2015 wakati wa kuahirisha Bunge Mheshimiwa Mrema alitoa maelezo ambayo sio sahihi alipoeleza kuwa mimi James Francis Mbatia niliwahi kusema kuwa yeye ni mgonjwa anayeugua maradhi ya ukosefu wa kinga mwilini yaani UKIMWI.
“Maelezo yote aliyoyatoa sio sahihi na sijawahi na sitawahi kutamka maneno hayo… Sijawahi kumnyanyapaa Mheshimiwa Mrema wala mtu yoyote aliyeathirika na maradhi ya aina yoyote“
“Mimi sina uadui na mtu yoyote akiwepo mheshimiwa Mrema hata sasa hivi amekaa kwenye kiti changu sina ugomvi nae.
"Nimezaliwa na nimekuzwa kwenye familia ya wacha Mungu siwezi nikafanya hivyo.. To grow old is mandatory but to be wise is optional…
“Mwaka huu ni mwaka wa uchaguzi Mkuu ni rai yangu kwa watanzania wote wachague vionzozi wenye uwezo, wacha Mungu, wakweli na wenye kuchukia propaganda, ubaguzi, chuki na ubinafsi.
“Baadhi ya viongozi wanadai kuwa wana hatimiliki ya maeneo wanayoongoza, dhana hii sio sahihi, nataka kuwahakikishia Watanzania wenye hatimiliki ya nchi yao ni Watanzania wenyewe“
Nimekuwekea Video Hapo Chini