Diamond Akanusha Kupewa Milioni 500 na Lowassa ili Ampigie Kampeni....Asema taarifa hizo zinalengo la Kumchafua Lowassa


Meneja  wa msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Nasib Abdul ‘Diamond’, Babu Tale, amesema hawajawahi kupewa kiasi cha fedha Sh mil 500 na Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, ili wampigie kampeni za urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).



Akizungumza na Mpekuzi, Babu Tale alisema watakuwa wehu kukataa fedha nyingi kiasi hicho wakati wenyewe wanafanya muziki ili kupata fedha, lakini ukweli ni kwamba hawajapewa kitu chochote.

Alisema hata hivyo Diamond yupo tayari kumfanyia kampeni mgombea yeyote atakayetangazwa kuiwakilisha CCM.

“Kama kweli tungekataa fedha hizo hata Mwenyezi Mungu angetulaani, ila naamini taarifa hizo zitakuwa zinasambazwa na wapinzani wa kisiasa wa kiongozi huyo kwa  lengo la kumchafua, hajawahi kutupa ofa hiyo,” alisema Babu Tale.

Meneja huyo alitoa ufafanuzi huo baada ya hivi karibuni kuzagaa kwa taarifa ambazo si za kweli, kwamba walipokea kiasi hicho ili kumpigia kampeni Lowassa.
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. na wewe domo ukijiingiza tuuu kwenye siasa umekwishaaaa, eti yuko tayari kumpigia kampeni mtu wa ccm, haya!!!

    ReplyDelete
  2. Watu wanatafuta hela babu! Million 500 ata wewe uie comment hapo ju huwei kuzikataa,or kwa kuwa mwenzio ndo unongee pumba,km ni mdomo kaumbwa na MUNGU na ww una mapungufu kibao,moja ya upungufu wao ni kukosa ustaarabu wa lugha ya kuongea na weznio....Diamond ukipewa hela ndefu km hiyo usiiwache wala nini..opportunities ndo hizo

    ReplyDelete
  3. Watu wanatafuta hela babu! Million 500 ata wewe uie comment hapo ju huwei kuzikataa,or kwa kuwa mwenzio ndo unongee pumba,km ni mdomo kaumbwa na MUNGU na ww una mapungufu kibao,moja ya upungufu wao ni kukosa ustaarabu wa lugha ya kuongea na weznio....Diamond ukipewa hela ndefu km hiyo usiiwache wala nini..opportunities ndo hizo

    ReplyDelete
  4. DIAMOND USHARI WA BURE NAKUPA USIKUBALI KUKIPIGIA KAMPAIN CHAMA CHOCHOTE CHA SIASA KWANI WEWE WAPENZI WAKO NI WA KUTOKA VYAMA VYOTE KWA HIYO SWALA LA SIASA MIYE NAKUSHARI KAA MBALI NALO ILI NYOTA YAKO IZIDI KUNGAAA. HIVI UNAFIKIRI MIYE MSHABIKI WAKO SANA NIKO CHAMA FULANI HALAFU WEWE UKIPIGIA KAMPANI CHAMA KINGINE??? SOO SIO BUSARA KWAKO KUJIINGIZA KWENYE SIASA. ZIACHE ILI UENDELEE KUWA JUU KWA WASHABIKI NA WAPENZI WAKO WOTE KUTOKA VYAMA TOFAUTI. BIG UP!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad