Dully Sykes Alaumu Wasanii Ambao Hawakuja Kumzika Baba yake

Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Dully Sykes, ameshangazwa na kitendo cha wasanii wengi kutojitokeza katika mazishi ya baba yake mzazi, Ebby Sykes

“Nilitegemea kwakuwa tunampumzisha baba yangu hapa hapa Dar es Salaam, wangekuja wasanii wengi ambao ni marafiki zangu, lakini hali ilikuwa tofauti kabisa,” .

“Sijui walijua nitakuja kuwaomba fedha zao, mimi nilishapata michango mingi kutoka kwa watu wengine mbalimbali, ukweli wasanii tuache roho za kimasikini,” alisema.

Sykes aliendelea kusema amegundua asilimia kubwa ya wasanii wamekuwa wakipendana wakati wa raha tu, lakini inapofika muda wa matatizo kila mmoja hukimbia.

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. ndugu umeshamzika baba yako funga domo, hata wangekuja wasinge mrudisha baba yako duniani, omba Mungu songa mbele.

    ReplyDelete
  2. ACHA KUONGEA ONGEA, mbona wakati wasanii wengine wanafiwa hukusema hivyo? ndo ushajua nani rafiki na nani mamluki. songa mbele, kwanza wewe sio wa kwanza kufiwa na baba. tumefiwa wengine toka tupo makinda. hivyo nakushauri kama mtu mzima, komaa na kazi utunze familia yenu. afu wewe DULLY MI NAKUPENDAGA SANA SIO MTU WA KUONGEA ONGEA, hivyo usibadilike tafadhali. tupo tunaokupenda LIFE GOES ON.

    ReplyDelete
  3. Jamani mwacheni aongeeee ili aondoe Stree zake. Unajua binadamu tumetofautiana katika kuondoa zile Stress hasa tunapokutana na mambo makubwa. Sasa huyo mjamaa yuko so much depressed juu kaondokewa na baba yake mzazi na that's the only way ya kuondoa hizo depression zake. Kuongea kwa sanaaaaaa na kubakia kulalamika lalamika......................Kijana ndio ukubwa huo. Kua uyaone.

    ReplyDelete
  4. Ukiona umetemwa msibani , ujuwe Na wewe Si mshiriki wa misiba ya wenziio ,,somo Hilo JIPANGE MR MISIFA

    ReplyDelete
  5. Somo Hilo. Ushirki misiba ya wenzio

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad