Lady Jaydee ameendelea kujibu maswali ya mashabiki wake kupitia Instagram, na maswali mengine aliyokutana nayo ni kuhusu kama ana mtoto au ameasili mtoto ambaye huonekana kwenye kipindi chake cha ‘Diary Ya LadyJaydee’ kinachorushwa kupitia EATV.
“SWALI: Una watoto wangapi?
JIBU : Sina mtoto wala watoto
SWALI:Utazaa lini?
JIBU : Sijajua mpk sasa nitazaa lini, ila siku yoyote ile ikitokea naweza kuzaa
SWALI: Kwanini huna mtoto /watoto?
JIBU : Sina mtoto /watoto sababu sijawapata, nikipata nitakuwa nao.
SWALI: Tunaskia ume adopt mtoto ?
Na mtoto tunaekuona nae ni wa nani?
JIBU : Sija adopt mtoto, mtoto mnae muona ana shine like a star, ananiita Shangazi, ninaishi nae sbb ya ukaribu wa shule anayosoma ,Tunaishi wawili tu, mimi na yeye
Anaitwa “Mokonyo Yvonne Mbibo” Ni binti wa mdogo wangu @dabomtanzania
SWALI: Tunaskia una mtoto mkubwa ulimzaa ukamuacha kijijini Shinyanga /Musoma
JIBU : Sina mtoto niliemuacha kijijini, sijawahi kuishi kijijini.
Sijawahi kuishi Musoma, kwetu ni Bunda na huwa naenda ikitokea misiba kuzika, sijawahi kuishi huko zaidi hata ya miezi 2 Shinyanga niliozaliwa ni mjini
Nilihama Shinyanga, kuja Dar es salaam nikiwa na miaka 11
Sijawahi kurudi kuishi huko tena zaidi ya kwenda kusalimia.
SWALI: Tunaskia huzai, ulitoa kizazi ili ufanikiwe kifedha?
JIBU : Sijatoa kizazi na sifanyi kitu chochote unusual ili kupata mafanikio
Angalizo : Mwenyezi Mungu hadhihakiwi, so stop calling me names. …….Kesho anaijua yeye, lolote pia linaweza kutokea. Accept me the way I am”
Lady Jaydee: Sina mtoto wala watoto, Sijajua mpaka sasa nitazaa lini…Accept me the way I am
8
February 18, 2015
Tags
Huyu dada naamkubali kupita maelezo. Ni mfano mzuri wa mtanzania halisi. Nadhani ametoka katika familia bora ndo maana hata mambo yake yanaenda kwa mpangilio. Akina wem na wenzake wangekuwa hata robo ya akili yake wasingeishi kama mahayawani. Kuna wakati unataman wasanii wengine kama niliowataja hapo na kundi lake wasijitambulishe kama ni watanzania kwan ni aibu. Wema popote ulipo unatukera sana tuliowengi ona mifano ya wenzako. Safi sana Jay d kwa kusambaza harufu yenye manukato ya hekima na akili ili kuwafundisha walioamua kujikabidhi kwa shetani. Uishi milele binti uliefunzwa na kutengenezwa. Tunakupenda b binti machozi
ReplyDeleteHivi hupati raha wala utamu bila ya kumtaja WEMA, anazungumziwa JIDE we unahamisha mada kwa 'BEATUFUL ONYINYE' !! Huna undugu na Wema, humjui, hakujui, hakuhusu pua wala mdomo, unakereka nini?? Akifeli kimaisha ni yeye na familia yake, akipasi pia ni yeye na familia yake, anakupunguzia au kukuzidishia nini???!! FANYA YAKO muwache na YAKE....upo???
Deletefgfgfgf
Deletenakupenda dada mpaka najiogopa ipo siku Mungu atakupa unachotaka maana yeye ndiye muheza wakila jambo,LUV U.
ReplyDeleteJudith, Mwenyeezi Mungu muweza wa yote ndio aliyewapa wao watoto na wewe ukakosa, umekuwa muwazi na kueleza hali halisi. Kila jambo lina wakati wake, siku moja utapakata mtoto wa kutoka kwenye tumbo laki. Nakutakia kila la kheri katika maisha yako, usitetereke katika imani ya maisha yako. Keep it up JIDE! Mmwaa.
ReplyDeleteJD usijali wakati wa Mungu ukifika utapata mtoto tu. Mungu hana kuchelewa na kama linakunyima raha faraja pekee ni kwake yeye. na uzuri unamjua Mungu vizuri sana na tambua anakupenda sana tena sana usimuache.
ReplyDeleteYes Jide ni mkali. nimependa maelezo yako umejielieza vizuri sana. napenda kazi zako kwa saana na jinsi unavyojiamini. maswala ya mtoto umejibu vizuri mno. hayo ni majaliwa ya mungu. miye naamini mungu atakupa tu wakati wake kwako ukifika. BRAVO JIDE!! WEWE KWELI NI KIOO CHA JAMII.
ReplyDeletemungu akujalie upate mume na mtoto wako!!! tupo pamoja
ReplyDelete