Maswali 10 Kuhusu Magaidi wa amboni Tanga

Hebu tujiulize maswali yafuatayo kwa tafakuri pana:
1. Gaidi alijirushaje pangoni na pingu mkononi? Tuliambiwa polisi walimkamata gaidi mmoja na akawapeleka mapango ya amboni kuwaonesha walipoficha silaha. Eti alipofika mapangoni akajirusha ndani. Kivipi alijirusha na alikua na pingu?

2. Na kama hakuwa na pingu, polisi wanapaswa kujieleza kwanini hawakumfunga pingu gaidi? Mtu mnamshuku kuwa gaidi mnambeba kama bwana harusi? Huyu alitakiwa pingu za mikono na miguu. Au pingu zipo kwa wafuasi wa ukawa wanapoandamana?

3. Kwanini askari wamezuia waandishi kufika eneo la tukio kupiga picha na kuchukua matukio? Wanahofia nini? Waandishi wa kenya wanaingia hadi somalia "kulipo kitovu cha ugaidi" na wanacover story, wakati mwingine wanafanya interview na viongozi wa al-shabab, sembuse hawa vibarua wa amboni? Kwanini polisi wanazuia waandishi?

4. Kwanini polisi wanavujisha rekodi zao za sauti kuhusu hawa waitwao "magaidi wa amboni?". Juzi nilisikiliza clip moja ya sauti kati ya mtu aliyejiita polisi akiongea kwa simu na askari mwenzie aliyeko tanga akimueleza juu ya magaidi hao. Jana imevuja clip nyingine ya askari polisi wakiongea kwa simu juu ya mikakati waliyonayo kuwamaliza hao magaidi. Hivi inaingia akilini mikakati kupangwa kwenye simu? Hakuna radio call? Na hata kama ni simu kwanini wavujishe? Hivi hawaoni kuvujisha ni kuuza ramani kwa adui? Mi naona huu ni usanii tu.

5. Kwanini askari aliyeuawa hajatajwa jina wala waliojeruhiwa? Wanaficha nini? Luteni rajabu mlima alipofia vitani huko drc vyombo vya habari viliripoti na akatajwa majina yake kamili. Baadae akaja kuzikwa kwa heshima kama shujaa aliyefia kwny mapambanno. Vp huyu aliyefia amboni mbona hatajwi? Tunaambia tu, askari mmoja amepoteza maisha. Nani huyo? Kama mnaweza kuwataja wanaofia vitani nje ya nchi huyu wa amboni vp??

6. Hao magaidi wameingia lini huko mapangoni? Na walikua wakifanya nini huko muda wote, mbona hawakuwahi kufanya uhalifu wowote hadi askari walipowatibua?

7. Hao magaidi wanakula nini siku zote huko mapangoni? Au ndio kusema kwenye mapango ya amboni kuna shopping centre kama 'mlimani city?'

8. Halafu mapango ya amboni yanasimamiwa na mamlaka ya makumbusho ya taifa. So kuna watumishi ambao wapo kule mapangoni kila siku. Kuna wahifadhi, kuna walinzi, kuna mkuu wa makumbusho na watumishi wengine. Hivi hawa watu hawakuweza kugundua magaidi walioingia? Au labda wakati magaidi wanaingia watumishi wote walikua likizo?

9. Kwanini chagonja na igp wanapingana hadharani? Voa jana wamemnukuu igp mangu akisema askari aliyekufa alikuwa ktk mapambano na magaidi. Lakini chagonja jana kaongea na media na kusema askari aliyekufa alipigwa ambush. Yani wakati wamemkamata adui wanampeleka huko mapangoni akawaoneshe silaha zilipo; ile kufika tu wakiwa hawajui hili wala lile wakashambuliwa na risasi kutoka mapangoni hivyo mmoja kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa. Sasa hapa tumuamini nani kati ya mangu na chagonja?

10. Taarifa za kusikitisha zilizotolewa na jeshi la polisi leo ni kuwa eti baadhi ya magaidi hao wamekamatwa na wengine wametoroka. Tehtehteh kweli hii sinema aliyeandika script atakua cha-gonja maana huyu jamaa ni hopeless kabisa. Wametorokaje? Wamepita wapi? Askari wetu wakiwa wapi? Au kuna barabara huko ndani ya mapango zinapita hadi somalia?

nashauri polisi wajipange upya wanapotunga sinema zao za kujaribu kuwahamisha watanzania kwenye mijadala muhimu. Na wakitaka sinema yao iaminike na watanzania, wamtafute mtu mwenye akili sana awaandikie script, sio kumpa 'kichaa-gonja'

i rest my case.. J.pili njema.


Malisa G.J || your partner in critical thinking.!
Tags

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Yani umesema yotee ndg yangu, hii ndio serikali ya kikwete. Rais hopeless kabisa na uongozi wake wote pia. Mungu ibariki TANZANIA ipate kiongozi muadilifu

    ReplyDelete
  2. Tumeshazoea majibu mepesi ya kupanga matokeo, hata katika kubwa kama hili bado tu!!

    ReplyDelete
  3. rais mkiaa sio kichwa amalize tu mda wake tumechoka watanzania mana watu wanateketea tuu yy hajari anaangalia masilahi yake..bado majeshi yanalinda usalama nchi za wengne kwetu watu wanavamiwa kila siku why wasieke wanajeshi tanzania wakalinda mana police useless kaz yao kula pesa zetu tukiwa na matattizo

    ReplyDelete
  4. Umesema,,, lakini swali no8 linajibika kirahisrahis kwamba mapango hay yanayoitw ya amboni si haya tunayoyafaham mm na ww yaani yale yanayotumika na shughuli za kitalii, laghasha mapango yanayozungumzwa hap yako umbali usopungua 4klm kutoka mapango ya kitalii ambako hakuna ulinzi wala usimamiz wwte zaidi ya vijan wachache walojiajir kuvunja mawe nakuyauza, hivo ndokusem ni semi small caves ambazo ziko porini

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad