Udaku Special Blog
Mimi ni mwanamke mwenye umri wa miaka 33 mume wangu ana umri wa miaka 41. Sote ni wasomi na wafanyakazi. Tumefunga ndoa miaka tisa iliyopita tuna mtoto mmoja ana umri wa miaka 7.Wakati tunafunga ndoa wote tulikua mabikra. Mimi nilikua sijawahi kuwa na mpenzi na mume wangu akuwahi kua na mpenzi..
Tulianza kushiriki tendo la ndoa siku ile tulipofunga ndoa. Kwa kweli kwa ujumla maisha yetu ya ndoa ni ya furaha kwa mambo yote lakini sio ya kiunyumba.
Mimi na mume wangu atujawahi kuwa mbali kikazi. Maisha yote hadi leo tuko Dar es salaam pamoja. Tulipofunga ndoa miaka ya mwanzoni tulikua tunaweza kukutana kimwili hata mara tatu kwa mwezi, miaka ilivyokua inazidi kwenda ikawa kukutana kimwili inakua mara moja kila baada ya miezi miwili na tukikutana ni bao moja tu.
Sasa hali imezidi kua mbaya kwani sasa imepita miezi sita tunalala kitanda kimoja mume wangu ajanigusa, hali hii inanisononesha kwani natamani mtoto wa pili. Kwakweli atuna ugomvi wowote. Mimi na mume wangu wote ni wacha Mungu.
Mume wangu ni mchapakazi sana tukitoka kazini tuko wote na sio mtu anaependa kwenda kutembea bila familia. Jumamosi na Jumapili mara nyingi tunatoka out tukirudi home akuna kinachoendelea, anageuka ukutani analala kama mtoto hadi asubuhi, wala hata anigusi nikimsogelea hata ashtuki.
Na asubuhi tukiamka tunaenda ofisini na akifika ofisini lazima anitumie message, mke wangu nakupenda sana. Simuelewi na nashindwa kumuuliza maana mimi kama mwanamke naona aibu.
Kwakweli mawazo ya kutoka nje ayapo kabisa kichwani mwangu maana simjui mwanaume mwingine zaidi yake pia namuogopa Mungu siwezi kucheat.Ila kwa hali ilipofikia naona bora nitengane nae niishi maisha yangu maana bila unyumba amna maana ya ndoa na nataka sana mtoto.
Wadau naomba ushauri je hii ni kawaida, nifanyeje.
ongea nae ujui tatizo ndo utaweza litatua vingivyo uongo wewe na yeye ndo wa kulimaliza hili
ReplyDeleteMlikuwa mnakutana Mara tatu kwa mwezi?huyo jamaa hanisi nn?njoo kwangu sitakuomba mchezo pale tu unableed?sasa piga mahesabu Kwa mwaka.
ReplyDeletekama kweli unaitaji ushauri sio kila kitu kinaandikika.weka namba tukupigie tukushauri.ukiona mtu analete mzaha unaitema simu yake.
ReplyDeleteInawezekana akawa na upungufu wa nguvu za kiume(uhanithi) ila Anonymous 01:31 ameizungumzoa vibaya. Jaribu kumtafutia tiba mbadala kabla hujaomba talaka. Tiba yenyewe ni vyakula vya kuongeza nguvu za kiume na hamu ya kufanya mapenzi. Ulizia kwa watu wa Pwani watakueleza ila nina amini km watu wa Pwani wana hivyo vitu basi hata Wabara nao watakuwa navyo. Pole sana mdogo wangu kila NDOA ina majaribu yake labda angekuwa hana hilo tatizo mngekuwa na watoto watano na huku ana nyumba ndogo 3. Nakuomba usikimbilie kudai talaka hujui huko utakutana na nini usije ruka mkojo ukakutana na puhpuh(shoga).
ReplyDeleteMtangulize Mungu kwa kila jambo lako ili maamuzi yako yawe ya busara.
Jambo la kwanza na la busara lilikuwa h kumbwambia huyo mumeo na kumuuliza nin shida.......kwanin watu wa siku hiz mmekuwa wa kuanika mambo ya ndoa mitandaoni??ni wazi mme wako sio mkorofi kwanin usizungumze nae taratibu....au kwanin usianzishe wewe game uone atafanyaje ili ujue hataki ama ana physical problemas whatsoever.
ReplyDeleteongea naye na kama vipi tafuta tiba la sivyo labda ana mcharuko na haujui.
ReplyDeletePOLE, ONGEA NAYE ILI IKIWEZEKANA MUENDE MKAWAONE MADAKTARI WANAOHUSIKA NA MAMBO KAMA HAYO. LA PILI UNAWEZA KUMUANZA WEWE KWA SABABU NI MUME WAKO, SIO LAZIMA YEYE NDIO AANZE. ALAFU UMESEMA UNAMUOGOPA MUNGU SASA TALAKA YA NINI? MUOMBENI MUNGU AU HATA IKIWEZEKANA MUENDE KWENYE MAOMBI MAANA ANAONEKANA ANA SHIDA, SI KAWAIDA KWA MWANAUME ALIYEKAMILIKA KUWA HIVYO.
ReplyDeleteongea nae tu ili ujue shida ipo wapi. mm pia nilikua na wa kwangu alikua tu akianza game uume unalala. tulikaa tukaongea na shida ilikua stres za kazi na mambo mengine ya hivo.. saiv we are fine nilimuelewa saiv stress hizo hazipo tena mambo kama kawaida. usipanic
ReplyDelete