Mke wa Mtu Anaswa Akifanya Mapenzi na Chemba Kwenye Gari Live

BIASHARA ya kuuza miili imezidi kushamiri katika viunga vya Jiji la Mwanza na mwanzoni mwa wiki hii Kitengo Maalum cha Oparesheni Fichua Maovu (OFM) cha Global Publishers, kilifanya zoezi lingine kubwa baada ya kumnasa mwanamke mmoja akifanya mapenzi ndani ya gari katika eneo la Kirumba, Ijumaa lina data kamili.

Baada ya kutajiwa maeneo yanayosifika kwa biashara hiyo maarufu kama uchangudoa, OFM ambao juzikati walilifumua danguro lililopo maeneo ya Liberty jijini hapa, Jumanne wiki hii lilifanya matembezi katika eneo hilo ili kubaini jinsi biashara hiyo haramu inavyofanyika.

Majira ya saa tisa za usiku, katika eneo lililopo jirani na Villa Park, OFM ilishuhudia wanawake wengi wakiwa wamesimama na kujinadi kwa wanaume waliokuwa wakiwafuata na kuzungumza nao biashara kama wauzao vitu halali.

Baadhi ya waliokubaliana waliondoka kuelekea kusikojulikana na wengine, walisogea pembeni na ‘kujisevia’ kwenye maeneo ya giza.Lakini katika hali ya kushangaza, mwanamke mmoja akiwa na mwanaume, alionekana akiingia katika gari moja lililokuwa limeegeshwa katika eneo linalojulikana kama Magereji, lililopo pembeni ya Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa na OFM lilipowafuatilia, liliwabamba wakifanya mapenzi.

Wakati wakianza kupigwa picha mfululizo, mwanaume alifanikiwa kukimbia kwa kupitia dirishani na kutokomea bila kunaswa na kamera, wakati mwanamke alijikuta katika fedheha kubwa na kuanza kuomba msamaha kuwa picha yake isisambazwe kwa vile ataaibika.

Ijumaa: Sasa kwa nini unafanya biashara hii?
Mke wa mtu: Ni shida tu jamani, mume wangu kanitelekeza, naombeni mnisaidie msinitoe gazetini maana ndugu zangu wala hawajui kama nafanya biashara hii?

Baadaye katika uchunguzi wake, OFM ilibaini kuwa mlinzi wa gereji iliyopo eneo hilo ndiye amekuwa akitoa nafasi ya makahaba hao kutumia magari yanayolazwa eneo hilo kwa kuwatoza kiwango cha fedha ambacho hata hivyo hakikufahamika mara moja ni kiasi gani.

Hata hivyo, uchunguzi wa OFM umebaini kuwa machangudoa wengi wanaojiuza katika vijiwe vya Mwanza, wanatoza kati ya shilingi elfu nane hadi kumi kwa huduma ya muda mfupi, wakati wale wanaohitaji kulala nao, wanalipishwa kati ya shilingi 25,000 hadi 30,000.

Ijumaa linalaani biashara hii na linawatahadharisha wanaoifanya kuiacha la sivyo yatawakuta makubwa ikiwa ni pamoja na kuaibika kwa picha zao kuanikwa gazetini.

GPL
------------------
Forgiving does not erase the bitter past. A healed memory is not a deleted memory. Instead, forgiving what we cannot forget creates a new way to remember. We change the memory of our past into a hope for our future.
By Lewis B. Smedes

Share Your Comment Below Using Facebook or Blogger Comment Box

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mshakaa na kufikiria nijinsi gani yakuwasaidia maana naona kazi yenu nikuwaabisha tuuuu wengine wanajikuta ktk hayo mazingira kutokana nachangamoto zamaisha tu,so msiangalie kuuza habari tu mkaemfikirie nikamsaada gani hatamawazo yanaweza kuwabadilisha

    ReplyDelete
    Replies
    1. wewe umesema sasa akiachwa nyie mnapata faida gaaaniiiiiii???

      Delete
  2. HALAFU NA NYIE ACHENI KUWADHALILISHA WANAWAKE TU IWEJE MWANAUME AKIMBIE MSIPATA HATA PICHA YAKE MOJA ?? HATA YA MGOGONI KUONYWESHA ANAKIMBIA???? HUYU ANAACHIKA HIVYO !!!!!! MNAMZIDISHIA MATATIZO!!!

    ReplyDelete
  3. haya anaachwa na mumewe je mnapata faida gani???????????????????

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad