Muswada wa Mahakama ya Kadhi Waondolewa Bungeni

Muswada wa Sheria ya kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi Tanzania Bara hautajadiliwa katika mkutano wa Bunge unaoendelea mjini Dodoma baada ya serikali kuuondoa kwa maandalizi zaidi.



Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju, alisema jana usiku kuwa wameamua kuuondoa muswada huo ili kupata fursa ya kutoa elimu zaidi kwa viongozi wa dini na kuufanyia marekebisho baadhi ya maeneo.

Alisema serikali inatarajia kuurejesha tena bungeni mwezi ujao. Hata hivyo, habari za uhakika kutoka Dodoma zinasema kuwa kulikuwa na mvutano mkali ndani ya kamati ya Bunge iliyokuwa inashughulikia muswada huo uliokuwa kwa misingi ya imani hivyo busara ilitumika kuahirishwa uwasilishwaji kwa mara ya pili kwani mjadala kwenye Bunge zima ungeweza kuleta mpasuko.

Muswada huo ulikuwa unawasilishwa kutokana na ahadi ya serikali kwenye Bunge Maalum la Katiba ambako mjadala ulikuwa mzito baadhi ya wajumbe wakitaka mahakama ya kadhi iingizwe kwenye Katiba Inayopendekezwa, lakini Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, akashauri kutungwa kwa sheria ya mahakama hiyo, badala ya kuuingiza kwenye katiba.

Tangu serikali itangaze kuwa itawasilisha muswada huo bungeni, kumekuwa na mvutano ndani ya jamii, kundi moja likiupinga kwa madai kuwa serikali haipaswi kujihusisha na masuala ya dini kama katiba inavyoelekeza. Ilielezwa kwamba kama Waislamu wanahitaji mahakama hiyo, basi waunde kwa njia zao wenyewe bila kuhusisha serikali.

Hata hivyo, serikali ilisema kuwa imeandaa muswada huo ili kuweka utaratibu wa kuundwa kwa mahakama hizo kisheria, lakini suala la uendeshaji wake na gharama hazitabebwa na serikali bali Waislamu wenyewe.

Tayari jumuiya za Kikristo kupitia maaskofu wao wamekwisha kutoa msimamo wao juu ya mahakama hizo wakisema kuwa siyo jukumu la serikali kuzianzisha.
Tags

Post a Comment

22 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. NDIO SIO JUKUMU LA SERIKALI NI LAO WENYEWE WAISLAMU NA HALITAKIWI KULETWA TENA BUNGENI.

    ReplyDelete
  2. Waislamu ni sehemu ya jamii hii kwahiyo serikali inawajibika kusimamia mambo yao na sio kipiga dana dana.

    ReplyDelete
  3. SERIKALI HAINA DINI !! ITASIMAMIA DINI NGAPI WEWE?

    ReplyDelete
  4. Mungu ni mwema atatutoa kwenye utata huuu!!!!

    ReplyDelete
  5. KAMA WANAONA MAHAKAMA YA KAZI WANAIPENDA KWANINI WASIANZISHE WAO WENYEWE SERIKALI NI KWA WATANZANIA WOTE IWEJE MASWALA YA DINI FRANI YAINGIZWE KWENYE KATIBA HIYO ITASABABISHA MPASUKO KATIKA JAMII VIONGOZI KUWENI MAKINI HUU NI MWANZO WA UBAGUZI "KWANI WAO WAJITENGE NA MAHAKAMA YAO WAKATI SHERIA ZA NCHI ZIPO" ALAFU ETI MAHAKAMA IWE KWENYE KATIBA ILA ITUMIE SHERIA ZA DINI NINI UMUHIMU WA KUWEKWA KWENYE KATIBA KAMA SIYO NCHI KUIWEKA CHINI YA DINI FULANI

    ReplyDelete
  6. Ni kweli kabisa si jukumu la serikali ni lao wenyewe WAISLAM kulianzisha na kulisimamia wao wenyewe na kwa gharama zao

    ReplyDelete
  7. Mahakama Ni chombo cha serikali na mahakama ya kazi razima itapitishwa kama serikali aina dini hayo matatizo Ni ya wakristo sisi tunayo na Ni uislam saga chupa ubwie laana tulahhi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Umekwama, kapitishe kwako

      Delete
    2. hajui asemalo asamehewa tu!!

      Delete
  8. Tatizo wakristo muwabinafsi na mna robot mbaya sana kila kitu mmehodhi nyinyi ktk nchi hii lkn hamtosheki iko kimahakama cha kadhi kinakutoeni mishipa ya shingo. Roho zinawauma khaa lol.

    ReplyDelete
    Replies
    1. hujui usemalo. nchi zote zenye mahamaka ya kazi ndio zilotawaliwa na vita mfano irani iraq palestina uturuki, yemen, libya jordan zote hizo kuna mahakama ya kazi imeshindwa kufanya kazi?? hapa tanzania hatuitaki kabisa itaanzisha migogoro familia zetu zina dini zote. Jamani epusheni shari!!!

      Delete
  9. mahakama ya kadhi ni tatito angalieni nchi kama somalia ilivyopitisha sharia machafuko yalimea sasa nchi hii isiyo na dini mahakama za kidini za nini jamani? au mmechoka amani msemege na mnao zitetea rudia angalia nchi zenye utawala wa kikadhi zinavy taabika naungana na mwanasheria kutouitisha muswada huo bungeni na waislamu mkae mfanye kadhi ndani ya misikiti sioni ni wapi wakristu walipo pendelewa hapoo

    ReplyDelete
  10. mahakama ya kadhi ni tatito angalieni nchi kama somalia ilivyopitisha sharia machafuko yalimea sasa nchi hii isiyo na dini mahakama za kidini za nini jamani? au mmechoka amani msemege na mnao zitetea rudia angalia nchi zenye utawala wa kikadhi zinavy taabika naungana na mwanasheria kutouitisha muswada huo bungeni na waislamu mkae mfanye kadhi ndani ya misikiti sioni ni wapi wakristu walipo pendelewa hapoo

    ReplyDelete
  11. Nafikiri mnatambua kinachoendelea nigeria hadi sasa, hayo yote ni kwasababu ya mgawanyiko wa kidini uliopo nigeria. Watanzania tusitake kufika walipo nigeria, swala la mahakama ya kadhi lisirudishwe bungeni, mahakama iliopo inajitosheleza kabisa sioni umuhimu wa kuwa na mahakama ya kadhi wakati mahakama ya taifa ipo. Kuwepo kwa mahakama ya kadhi kutaongeza uhalifu, vitendo vya ukatili na ubaguzi wa kijinsia na serikali itashindwa kuwaadhibu watu watakao kuwa wakifanya vitendo hivyo endapo watakuwa ni waislamu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. ni kweli kabisa hii mahakama ilaleta machafuko kama somalia walivyoanzisha sharia mambo yamezidi kuwa mabaya hivi mnajifanya hamuoni wala kusikia??? mahakama ya kadhi noooo. fungue huko huko misikitini kwenu msiihusishe serikali haina dini.

      Delete
  12. Tatizo nyie wakristo mnaogopa kukatwa vichwa hatutawakata nyie ndugu zetu sisi tutafanya mambo yetu kwa amani kabisa.

    ReplyDelete
  13. Haina haja hata ya kubishana kwa haya, yanayojili katika ulimwengu huu yote yako wazi, huu ulimwengu toka enzi na enzi binadamu, siku zote upishana, huyu anajion anjua kushinda huyu, na huyu anajiona anajua kushinda huyu, wanayoyatafuta leo ndio matunda ya baadae yakiwa mabaya mazuri ndio hivyo tena, binadamu tumetofautiana kimawazo, na kila kitu, wewe unawaza mazuri mwenzako anawaza mabaya, lakini ni binadamu huyo huyo, hiii nchi haina dini, kila mtu ana uhuru wake wa kuamini, wengine wanawarazimisha wengine, ni vitu viwili tofauti, matokeo yake,ipo mifano mingi hasa huku huku Africa, ndio kwenye matatizo lukuki, kwa kuwa tumeshindwa kupambanua mambo yetu wenyewe, mpaka tuangalie mbona wale wanafanya hivi, nasi hivyo hivyo hata kama mabaya,

    ReplyDelete
    Replies
    1. mahakama ya kadhi anzisheni huko huko msikitikini kwenu hakuna mtu anawazuia lakini iweke kwenye katiba nooooooooooo .nchi hii itavurugika kabisa. wanasema ukiona mwenzio ananyolewa nawe tia maji. tuonaona yanayotokea somalia misri palestina uturuki,nigeria sudan zote hozo ni kwa ajili ya mambo ya sharia. hivi muambiweje mpaka muelewe?????????

      Delete
  14. Ivi. Ktk.Ramani ya DUNIA kuna. Inchi. Inayoitwa Vatican mbona ubalozi wke upo hapa Tanzania na memorandum of understanding baina ya makanisa na serekali Jee huo cio udini au roho mbaya turn inawasumbua wakristo na jee better chance aliyoahidi nyenyere Julius kambarage kuyapa makanisa na akayapa jee huo cio udini? Acheni roho mbaya wenzetu wakristo khaa lol.

    ReplyDelete
    Replies
    1. huo wivu usiokuwa na maana.

      Delete
  15. Na izo inchi mnazozitaja kuwa zina vurugu ivi nikweli hamjui chanzo cha vurugu hizo au mnajipumbaza tu? Acheni. UNAFIK HUO.

    ReplyDelete
    Replies
    1. alaa kumbe unajua chanzo cha vurungu?? tuambie siye hatujui kabisa!!

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad