Mzee Yusuph kuoa tena mke wa watatu,Wake zake watupiana vijembe mtandaoni


Mwimbaji mahiri wa muziki wa Taarab nchini ambaye pia ni mkurugenzi wa kundi la Jahazi Modern Taarabu,Mzee Yusuph anatarajia kuoa tena mke wa tatu hivi karibuni huku wake zake wawili wakiwa kwenye bifu zito wakitupiana vijembe mtandaoni.

Akipiga stori na Uheard na Soudy Brown alisema kuwa anatarajia kuoa mke huyo ambaye anaishi huko visiwani Pemba,na kwamba mipango ikiwa tayari kila kitu kitakuwa hadharani.

Hivi karibuni wake zake wawili ambao ni Malkia Leila Rashid ambaye pia ni mwimbaji wa kundi hilo na mke wake mdogo aitwaye Chiku wamekuwa wakirushiana vijembe kwenye mtandao wa kijamii wa ‘WathsAAp’ kwa kuandikiana ‘Status’ za vijembe.

Habari zinasema kuwa wake hao wamekuwa kama chui na paka na mzee Yusuph hana mpango wa kuwapatanisha kwa kuwa hakuna hata mmoja aliyeonyesha chuki kwa mwenzake akiwa na nao.

‘’Waache tu warushiane vijembe tena ndiyo vizuri na dawa yao nawaletea mke wa tatu na wala sina mpango wa kuwapatanisha,"alisema Mzee Yusuph.

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. KAA BABA HUTOSHEKI!!!!! ??

    ReplyDelete
  2. UNAONGEZE DOSE YA KULISHWA UCHAFU!!!

    ReplyDelete
    Replies
    1. NI KWELI KABISA ANAONGEZA DOSE YA KULISHWA UCHAFU!!

      Delete
    2. UTAKUNYWA MIKOJO WEEE MPAKA BASIIII

      Delete
  3. kuoa mkwe wa tatu ujinga huo!!!!wewe unadhani unawakomoa! unajikomoa mwenyewe. wazungu wanasema THINKI TWAISI BEFOO YU DU!!!

    ReplyDelete
  4. Kweli baba huridhiki!

    ReplyDelete
  5. lol english is a big problem in bongo...., Think twice before you do nd nt vic verser

    ReplyDelete
  6. wee acha ushamba kwa akili yako umeona ni problem!! mwandishi kaamua tu kufurahisha.
    zinaandikwa sana kwa mtindo huu

    ReplyDelete
    Replies
    1. mwambie, kiingereza na yeye wapi kwa wapi na wala hana asili nacho kwao, namtumbo.

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad