Mkuu wa Kituo cha Polisi Afungwa Jela Miaka 30 kwa kosa la Kumbaka Mahabusu

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa ya Njombe, imemhukumu aliyekuwa mkuu wa kituo cha Polisi Ilembula kifungo cha miaka 30 jela, baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka  mtuhumiwa aliyekuwa ndani ya mahabusu.

Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu Augustine Rwezile, baada ya mshtakiwa huyo James Nyambenga kukiri kosa hilo mahakamani, ambapo mshakiwa huyo anadaiwa kumtoa msichana huyo kwenye chumba cha mahabusu alikokuwa anashikiliwa na kumbaka.

Mwanamke huyo ambae ni mhudumu wa bar alikuwa anashikiliwa kwenye mahabusu ya kituo hicho kwa tuhuma za uzururaji.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu Rwezile amesema ushahidi uliotolewa na upande wa mlalamikaji na vielelezo vya daktari aliyempima msichana huyo viliweza kuithibitishia Mahakama kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo.

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. NDIO VIZURI SANA IWE ONYO KWA ASKARI WENGINE!!!

    ReplyDelete
  2. Vitendo vimezidi iwe fundisho kwa askari na wengine wote hongera hakimu wetu

    ReplyDelete
  3. Mambo mengine bwana!

    ReplyDelete
  4. Mambo mengine bwana!!!!

    ReplyDelete
  5. HUYO ALIM-MAIND TANGU ZAMANI. KWA HIVYO SIKU HIYO AKATUMIA UBOSS NA CYO URAFIKI. POLE YAKE. ANGEOMBA ANGEPEWA, CYO KUBAKA.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad