Hata hivyo, Profesa Tibaijuka alikana mashitaka hayo, na kusisitiza kuwa hakukiuka maadili hayo ya viongozi wa umma, kwa kuwa fedha hizo hakuziomba kwa maslahi yake binafsi, bali kwa ajili ya kuendeleza na kuboresha taasisi yake inayotoa huduma ya elimu kwa watoto wa kike wasio na uwezo lakini wenye vipaji.
Akimsomea mashitaka hayo mbele ya baraza hilo, Mwanasheria wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Wemaeli Mtei alisema Profesa Tibaijuka ambaye ni kiongozi wa umma, alishawishi na kuomba fedha na baadaye kupokea Sh bilioni 1.6 kutoka kwa James Rugemalira na mkewe.
Aidha, Sekretarieti hiyo kupitia shahidi wake ambaye ni Katibu Msaidizi wa Idara ya Viongozi wa Siasa kutoka Sekretarieti hiyo, Waziri Kipacha, alisema kupitia Kamati ya Uchunguzi iliyoundwa na sekretarieti kufuatilia sakata hilo, ilibaini kiongozi huyo aliomba na kupokea fedha hizo kupitia barua aliyoandika Februari 4, mwaka 2012.
“Tulibaini kuwa fedha alizoomba mlalamikiwa zilitumwa kwake kupitia akaunti yake namba 00120102640201 ya Benki ya Mkombozi iliyopo St Joseph jijini Dar es Salaam,” alisema huku akikabidhi baraza hilo barua hiyo ya Tibaijuka ya kuomba fedha na taarifa za kibenki kama ushahidi.
Alisema pamoja na hayo, kamati hiyo pia katika uchunguzi wake ilibaini mlalamikiwa ni mmoja wa wadhamini katika Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Barbro Johansson Girls Education Trust, ambapo barua kutoka Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA), ilithibitisha suala hilo. Na kwamba wamiliki wa shule hiyo ndiyo wadhamini.
“Tumebaini kuwa mlalamikiwa alipokea kiasi hicho cha fedha na wadhifa aliokuwa nao kama Waziri, jambo lililomwingiza katika mgongano wa kimaslahi,” alisema.
Alisema kitendo cha mlalamikiwa kupokea fedha hizo na kuingizwa katika akaunti yake binafsi, ni kosa kwa mujibu wa masharti ya maadili ya viongozi wa umma kwa kuwa viongozi wa umma hawaruhusiwi kuomba fedha au msaada au kujipatia maslahi ya kiuchumi au kumpatia mtu mwingine maslahi hayo ya kiuchumi.
Wakili wa Tibaijuka, Dk Rugemeleza Nshara, alidai mbele ya Baraza mteja wake hakuna kosa alilofanya, bali alitumia wadhifa alionao kama viongozi wengine akiwemo Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuomba na kuchangisha fedha kwa ajili ya maendeleo ya wananchi na si binafsi.
“Nataka kuuliza Baraza hili, ina maana juzi Waziri Mkuu, alivyoongoza uchangishaji fedha kwa ajili ya maendeleo alikwenda kinyume na maadili ya uongozi?,” alihoji.
Profesa Tibaijuka, alikiri kuomba fedha hizo kwa ajili ya kuendeleza taasisi hiyo yenye lengo la kujenga shule za mfano za wasichana wenyewe vipaji kila kanda ili kukuza na kuimarisha elimu ya mtoto wa kike nchini.
“Huu si msaada wa kwanza, tumekuwa tukifadhiliwa na Serikali ya Sweden kupitia msaada tuliopatiwa na Rais mstaafu, Benjamin Mkapa, ambaye alitambua juhudi zetu na kutuunga mkono, tumechangiwa na taasisi za ndani na nje na watu binafsi, kiasi kinachohitajika kuboresha shule hizi ni dola za Marekani milioni 14 sawa na takribani Shilingi bilioni 25.2,” alisema.
Alisema pamoja na Rugemalira aliyetoa Sh bilioni 1.6, pia mfanyabiashara maarufu nchini, Reginald Mengi alichangia taasisi hiyo Sh milioni 278, ikiwemo Serikali ya Sweden iliyomaliza mkataba wake iliyochangia Sh bilioni 8.1.
“Sisi tuliopo kwenye taasisi hii, tunaaminiana na ni waadilifu ndiyo maana fedha nilizoomba ziliingizwa kweli kwenye akaunti yangu lakini niliziwasilisha, zilizobaki ni deni nililokuwa naidai taasisi, lakini pia nimekopa Benki M Sh bilioni mbili kwa ajili ya kuboresha taasisi hii na kuweka dhamana nyumba yangu iliyopo Oysterbay. Mbona hili hamlioni?,” alihoji.
Wakati akijitetea, Tibaijuka aliomba akabidhi andiko lake mbele ya baraza hilo. “Nina andiko langu na naomba nilikabidhi, kabla hujafa hujaumbika, nasimama hapa leo kwa sababu tayari nimeshahukumiwa bila kusikilizwa, niliomba hata bungeni nipewe nafasi lakini nilihukumiwa kama Waziri nikavuliwa madaraka, nashangaa leo nimesimamishwa hapa kama mbunge,” alisema.
Alisema “mimi mpaka sasa nasema sijakiuka maadili labda wanasheria wanieleweshe kwa sababu nilisimama kama mimi wakati wa kuomba fedha na si kama waziri au mbunge, hivyo sasa naona lengo ni kunivunja moyo, kunidhalilisha, kunifanya kama mwanamke mhuni na tapeli.” Aliendelea kujitetea
"Nimekuja kujieleza ila.. Mimi siyo mwanasheria ila ukweli sina kosa na ndiyo maana nyaraka zote ambazo zipo hapa, mimi ndo nimewapa, nimekuja hapa kwa nia njema na naamini kwamba Baraza hili litanisikiliza kwa sababu ukweli ndiyo mwanzo wa maadili, lazima tupiganie haki na tupiganie ukweli.
“Kama mimi nimefanya kosa kusimama kuwasaidia watoto wenye vipaji ni kosa, naomba mwanasheria anieleweshe na naomba ukweli usimame maana tukienda na fitina peke yake, hatutafika. Mimi ni profesa na mchumi na ni mstaafu wa muda mrefu na nina pensheni, sina makuu, maisha yangu ni ‘simple’ (ya kawaida) huwezi kunikuta Dubai... Ila nipo tunafanya maendeleo na wananchi wangu,” alisema.
Hata hivyo alisema fedha anazodaiwa kuhamisha baada ya kupokea na kukatwa za kulipa deni la Benki M, zilizobaki zilikuwa ni halali yake kwa kuwa alikuwa akidai shule hivyo fedha hizo zilizobaki ni kwa ajili ya matumizi yake binafsi.
“Mimi ni mchakarikaji, mtafuta fedha na kiongozi anayeshindwa kutafuta fedha kwa ajili ya watu wake hafai.
"Hivyo nilipolipwa milioni 117 (Shilingi), nilitoa milioni mbili nikachangia Kanisa la Makongo na nikatoa laki nne nikapeleka kanisani na milioni 10 niliitoa kwa ajili ya matumizi yangu ya kununulia mboga, “ alisema.
Shahidi wa Profesa Tibaijuka ambaye ni Mjumbe wa Bodi ya Wadhamini wa Taasisi hiyo, Balozi Paul Rupia katika ushahidi wake mbele ya Baraza, alisema fedha hizo zimetafutwa na Profesa Tibaijuka.
Alisema aliitaarifu bodi kwamba zipo fedha zimeingia katika akaunti yake na zinatakiwa kulipa madeni wanayodaiwa. Alisema katika kikao hicho cha kutoa uamuzi wa kugawanywa kwa fedha hizo kilichofanyika Luguruni , hakuhudhuria, ingawa alikuwa na taarifa zote za kinachoendelea.
Rupia alisema bodi hiyo haikumpa masharti yoyote Profesa Tibaijuka ya kumaliza kulipa madeni hayo kwa sababu hawakuona sababu ya kumfuatilia kwa kuwa walimwamini, kutokana na juhudi zake binafsi za kupata fedha hizo. Shauri hilo lilianza saa 3 na baadaye kuahirishwa kwa muda hadi saa 6.30 mchana, lilipoanza kusikilizwa tena na kumalizika saa 11.45 jioni.
Katika shauri hilo, Profesa Tibaijuka alitoa ushahidi kwa zaidi ya saa tatu, akilalamika kuonewa na kuhukumiwa bila kusikilizwa. Shauri hilo liliahirishwa hadi Machi 13 mwaka huu, kutokana na muda kutotosha. Wakili aliomba udhuru wa kwenda Marekani kwa siku 10 na Jaji Msumi alikubali.
Jaji Msumi alisema wajumbe watapitia shauri hilo na siku hiyo itaamuliwa, endapo hukumu itatolewa wazi au kwa uamuzi wa ndani
----------------
The art of war is simple enough. Find out where your enemy is. Get at him as soon as you can. Strike him as hard as you can, and keep moving on.
Ulysses S. Grant
wewe mama mzima kweli wewe, umetumia MILIONI KUMI kununua MBOGA!!! mboga gani hizo, huyu mama kachanganyikiwa huyu!!!
ReplyDeleteMboga tuu au msemo wake wa kukejeli
ReplyDeleteNDO WALEWALE WA VIJISENTI UMESAHAU MZEE WETU WOTE WAKISHAPATA NDO DHARAU INAKUJA PALE
DeleteVijisenti
ReplyDeleteJAMANI JANA NIMEONA MTU KAVAA TISHET IMEANDIKWA maisha bora kwa kila mtanzania HALAFU ANANUNUA MIGUU YA KUKU 2 KWA SHILIINGI MIA 2 NA KWENDA NAYO HOME KULA NA UGALI!!!LEO MTU ANASEMA MILLIONI 10 ZA MBOGA?? MBONA MADHARAU MAKUBWA SANA!!! maisha bora sio kwa kila mtanzania!!!! ni kwa viongozi tu
ReplyDeleteHUO NDIYO MSEMO WA MTU ALIYESHIBA HUWA MANENO MACHAFU KAMA HAYO
ReplyDeleteWEWE UMESEMA KWELI ALIYESHIBA HAMJUI MWENYE NJAA!! MWENZIO ANAHANGAIKA KUPATA MIA 2 YA KUNUNUA MIGUU YA KUKU WEWE USEME 10 M KWA MBOGA TU JAMANI MUWE NA HURUMA BASI HATA KIDOGO!!
DeleteUMEME WENYEWE AMBAO NDIO HIZO 10 M ZA MBOGO ZILIKOPATIKANA TUNANUNUA WA ELFU ELFU TU SIKU UKINUNUA WA BUKU MBILI UNAJIONA TAJIRI JAMANI!!!MWENZIO 10 M ZA MBOGA TU KAAA!!!
DeleteYaani bara hili linaviongozi Collapt, wanataka uongozi, kama hawaelewi maana ya uongozi nini?, wao wanachowaza uongozi ndio njia ya kupatia utajili, wanaiba kila kitu cha mali za umma, mpka kodi, mwisho wa siku tunabaki kuitwa mataifa masikini, alafu wao na familia zao wanaishi, maisha bora na ya juu, wewe ulie huku chini, tena unaechangia pato katika taifa, na familia yako mnangaika, yaani imekuwa raia wa kawaida tunawangaikia wao na familia zao waishi maisha bora, tunawalisha na kuwahudumia, alafu wala hawana habari na sisi, wao ni wizi na ufisadi, maisha bora yamekula kwako, kwa kuweka hela za kodi na mali ya umma mifukoni kwao
ReplyDeleteWanaochangia hoja wapuuzi sheria ya maadili ni zee imetaja ukipewa Elfu Hamsini hivi leo Elfu Hamsini ni hela ila kesi hii tutajua mbivu na mbichi ni kupakana vinyesi Wezi wauza madawa ya kulevya na wanaomaliza tembo na kuua Albino wanajidhihirisha bila kufanya uchunguzi
ReplyDeleteFedha za ESCROW ni zaidi ya Bilion 300 mbona wamemshupalia huyu mama jamani? Halafu anachosema wala hawamsikilizi. Nendeni mkatembelee shule inayomfanya apate hii aibu tuone kama mtaendelea kumdodosa. Viongozi wanaiba na kula na familia zao tu ila yeye kwa kweli anatumia kwa maendeleo ya watu pia. Sweden wanamheshimu kama nini nyie waTZ ndio mnamdharau na kumdhalilisha. Akisema fedha ya mboga ni kulingana na fedha aliyopokea sio kwa dharau. Yaani mmekazana kukosoa tu kila anachosema. Kwanza mwacheni jiulizeni fedha zingine za ESCROW ziko wapi? kweli mnafungwa macho WaTZ. Huyo Chenge na Tiba wakikasirika waanze kusema ukweli wa ulaji wa viongozi ndio mtatafuta pa kujificha,
ReplyDeleteAnna usikubali kufa peke yako sema usiogope sema!!