Udaku Special
SIKU chache baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba na wafuasi wake kupigwa na polisi, Rais Jakaya Kikwete amesema tukio hilo limetokea kwa sababu
nchi inaongozwa kwa sheria na atakayekiuka atakumbana na mkono wa sheria.
Rais Kikwete alitoa kauli hiyo jana Ikulu jijini Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari baada ya kufanya mazungumzo ya faragha na mgeni wake, Rais wa Ujerumani, Joachim Gauck, ambaye yuko nchini kwa ziara ya siku tano.
Kabla ya Rais Kikwete kutoa kauli hiyo, Rais Gauck aliimwagia sifa Tanzania kutokana na namna inavyofuata utawala wa sheria, uhuru wa vyombo vya habari na kulinda haki za binadamu.
Baada ya viongozi hao kuzungumza mbele ya waandishi wa habari juu ya ziara hiyo, waandishi walipewa fursa ya kuuliza maswali na ndipo mmoja wa wanahabari kutoka Ujerumani, alipotaka kauli ya Rais Kikwete na Rais Gauck, juu ya msingi wa uhuru wa vyombo vya habari na haki za binadamu nchini, wakati hivi karibuni gazeti la The East African lilifungiwa na wanachama wa CUF kupigwa na polisi walipotaka kuandamana.
Akijibu swali hilo, Rais Kikwete alisema: “Tuna sheria zinazoongoza mambo hayo, huwezi kuamka tu ukaamua kuandamana, tuna taratibu zetu za vyama vya siasa kukusanyika, wala hatubani haki na uhuru wa wapinzani, ukivunja sheria hiyo utawajibishwa.
“Na hapa wapinzani ndio wanafanya mikutano mingi kuliko chama tawala, ikitokea hawajafuata taratibu, hatuwezi kuwaacha waendelee kuvunja sheria,” alisema Rais Kikwete.
hata kumpiga mtu akiwa tayari ndani ya defender???
ReplyDeleteKWELI KUNA MMOJA ALIKUWA ANAPIGWA AKIWA KWENYE GARI TAYARI!!
ReplyDeleteKuna siku anayoijua Mungu CCM itakuwa Oposision part kwenye nchi hii na mtakumbuka mambo haya
ReplyDeleteYaani ni aibu kwa mtu kama Rais kujibu jibu la kisenge kiasi hicho!
ReplyDeleteNI SHERIA GANI INAYORUHUSU POLISI KUPIGA MWANANCHI KAMA HAJAFANYA UHARIBIFU AMA KUKIUKA SHERIA?
JAMAN HAYA MANYANYASO MPAKA LINI JAMAN?SIJAWAHI KUONA OPPOSITION WAKIANDAMANA NA KUACHWA KWA AMAN ILA NI MAANDAMANO YA CCM TU
JAMAN SERIKALI MNANYANYASA WANANCHI WENU NA HUO NDIO UKWELI,
JARIBUNI KUIGA HATA NCHI ZA WENZETU WANAVYOKABILIANA NA MAMBO KAMA HAYA!
MMEACHA KUVAMIA KINA LUGAMALIRA HUKO KINA CHENGE MNAENDA KUVAMBIA WATU WENYE MAPENZI MEMA NA NCHI
OVYO SANA NA NI AIBU KUBWA TU MXEEEEEEEW
Labda vizazi vipya ndio vitaipindua ccm, ila upinzani bado sanaaaa bongo hata wakiungana issue ni uroho wa madaraka na ruzuku za uchaguzi,, ukawa wawe na nia moja wataweza, sio unafiki waliokuwa nao,,
ReplyDeleteRais wangu mbona mkutano ulifanyika kwa mara ya pili na hapakuwa na vurugu zozote? Inamaana sheria inaruhusu askari kumpiga raia hata kama amekubali kuingia kwenye defender kwa hiari yake? Hapa ndipo police wanapojenga chuki kati yao na raia.
ReplyDeleteSheria msumeno
ReplyDeleteipo siku na wewe yatakupata ndo utajua ni msumeno au nyundo
Deletekwanini rais hakuwa specific sheria ipi ilikiukwa na ni kwa naman gani? kuliko kusema 2 sharia shaeria zipo nyingi bhanaaa na sheria si mipasho.
ReplyDeletekashika mpini ipo siku wanao watashika makali
ReplyDelete