Rais wa Chuo cha CBE Ndani ya Ufisadi Mkubwa , Abambwa na Mamilion ya Pesa Chumbani Kwake

KIMENUKA! Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo cha Biashara (CBE), Ramadhan Kirungi amejikuta akiwa korokoroni ya Kituo cha Polisi cha Daraja la Salenda jijini Dar baada ya kudaiwa ‘kufoji’ saini ya benki ya wanachuo na kuchota shilingi milioni 31.

Kwa mujibu wa chanzo makini, wizi huo unadaiwa kubainika baada ya makamu wake, Godfrey Modest kutumwa benki kwa ajili ya kutoa fedha ambazo cheki yake ilishasainiwa.“Yule makamu aliporudi chuoni alimweleza mhusika, akashagaa sana na hakuamini kilichotokea ndipo walipoamua kumkamata rais huyo.

“Walipokwenda kumkagua kwake walimkuta na shilingi milioni 16.5 keshi zilizosalia zikiwa zimefungwa katika mafungu matatu,” kilisema chanzo chetu kikiomba hifadhi ya jina lake.

Baada ya habari hizo kutua kwenye Gazeti la Amani, mapaparazi wetu walimtafuta msemaji wa chuo hicho, Leonidas Tibanga ambaye alikiri kutokea kwa wizi huo na kuongeza kuwa hatua zimechukuliwa na mtuhumiwa alikamatwa na kupelekwa polisi huku uchunguzi zaidi ukifanyika.“Ni kweli wizo huo umetokea na hivi ninavyozungumza na wewe, mtuhumiwa yupo polisi lakini uchunguzi zaidi unaendelea,” alisema Tibanga.

Post a Comment

13 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. duh hatareeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee

    ReplyDelete
  2. yaani huyu ni mjinga sana huwezi iba halafu ukakaa hapohapo wakukamate

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe mzoefu sana,na zitakutokea puani siku si nyingi kama ilivyotokea kwa huyu mjinga mwenzio.Jasho la mtu huwa haliendi bure,Pumb................

      Delete
  3. Hao ndio tunaowategemea wamalize vyuo waje kuwa viongozi wasomi, duh kazi ipo urais wa chuo tu mshkaji ushapiga dili la mamilion sasa ukipata ukurugenzi si idara itafungwa kabisa.

    ReplyDelete
  4. Hao ndio UKAWA wetu,nao ni XCROW tupu!

    ReplyDelete
  5. Tanzania is a very very beautiful country lakini watu waishio ndani ya hii ni wabaya kiroho kitabia kifikira na ndio maana tuliamua kuondoka huko katika nchi yetu tunayoipenda watu husema "enough is enough"kuna siku utawaka moto na hapo ndipo watu wataheshimiana kisawsawa kama nchi nyingine zilizotokewa na hayo mambo"wengi wape usipowapa kuna siku watajichukulia wenyewe nguvu at any cost so beware you all wicked people

    ReplyDelete
  6. Bongo pakija kuwaka moto kisawasawa na moto ukizimika hapo ndiyo haki itatendeka lakini si vinginevyo hata aje Rais gani au Chama gani hakuna atakaye ishinda nafsi yake asiwaibie wabongo no way!they are all damn greedy mtu ana elimu duni anapewa ubunge sasa unategemea maendeleo gani toka kwa mbunge au kiongozi dizaini hiyo?

    ReplyDelete
  7. Hili li Rais litakuwa kada la maCCM

    ReplyDelete
    Replies
    1. hapana litakua chadema wapenda masifa

      Delete
  8. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  9. Ufisadi everywhere, hata waziri mpya pale port anataka kubadilisha uongozi ili apige.

    ReplyDelete
  10. safi kijana kila mtu anakula ofisini kwake

    ReplyDelete
  11. Dah!!pole mwanangu dili imebuma sio mbaya kushindiwa vitani.,ila godfrey modest nakuonea huruma lazima wazee wa kazi wakujumanne tevezi unaharibu dili za watu???uuuuuuuuwiiiiiiiiiii naliaaeeeee ungetulia tu kwani uliona utazurumiwa aaiiyaaaaaaa.,lazima wakuoe masela ukwepi labda ujifukie chini mana ht nje ya bongo hutoki umejiharibia kila kitu,ckutishi ila huo ni mtandao wa mamafia sio mtu mmoja.,pole KIRUNGI mwana we jembe ndo wanaotakiwa kuwa viongozi....

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad